Hakuna mchezaji yoyote aliyefukuzwa kwenye timu baada ya kupoteza mchezo dhidi ya Mgambo Shooting mwishoni mwa wiki, taarifa hizo zinasambazwa kwa Propaganda ili kuweza kuvunja umoja uliopo ndani ya timu kwa wachezaji na walimu pia kwa Viongozi na wanachama.Uongozi wa klabu ya Young Africans unasikitishwa na taarifa zinazotolewa na baadhi ya Vyombo Vya Habari tangu siku ya jumatano kwamba wachezaji Juma Kaseja, Kelvin Yondani, Athuman Idd "Chuji" wamefukuzwa kwenye timu na Emmanuel Okwi ameondoka kurejea kwao nchini Uganda ni za uongo mtupu.
Kelvin Yondani hakuungana na wenzake kambini baada ya kuomba kupumzika na kutatua matatizo yake ya kifamilia, Benchi la Ufundi walimpa ruhusa hiyo kwa kuzingatia mchezaji mwenyewe asingeweza kutumika kwa mchezo wa jumapili dhidi ya JKT Ruvu kufuatia kuwa na kadi tatu za njano, ataungana na wenzake mara baada ya tu ya mchezo huuo.
Athumani Idd "Chuji", David Luhende pamoja na kiungo Haruna Niyonzima ni wagonjwa, wanaendelea na matibabu kuhakikisha wanakua fit na kuungana na wachezaji wao mara baada ya mchezo wa siku ya jumapili.
Juma Kaseja yupo kambini pamoja na mlinda mlango Deo Munish "Dida" aliyekua majeruhi kwa takribani wiki tatu kufuatia kupata jeraha katika mkono wakati timu ikijiandaa na mchezo dhidi ya Mtibwa Sugar.
Emmauel Okwi yupo jijini Dar es salaam akiendelea na matibabu kufuatia kutonesha goti katika mchezo dhidi ya Mgambo mwishoni mwa wiki, awali Okwi aliiumia katika mchezo dhidi ya Prisons na kutolewa nje na machela.
Okwi akiongea na katibu mkuu wa Yanga Beno Njovu leo ofisini makao makuu ya Klabu ya Ynaga, amesema anaendelea vizuri na ataaungana na wenzake mara baada ya mchezo wa jumapili, lakini akisikitishwa na habari zilizotolewa juu yake amabazo hazina ukweli wowote.
Kufuatia wachezaji hao kushindwa kuungana na timu siku ya jumanne katika mazoezi ya jioni, kocha mkuu Hans Van der Pluijm alichagua wachezaji 20 ambao wap kambini kujiandaa na mchezo huo:
Magolikipa: Juma Kaseja, Deo Munish "Dida" na Ally Mustafa "Barhez"
Walinzi: Juma Abdul, Mbuyu Twite, Ibrahim Job, Raja Zahir ,Oscar Joshua na Nadir Haroub "Cannavaro"
Viungo: Frank Domayo, Said Dilunga, Nizar Khalfani , Salum Telela na Hamis Thabit
Washambuliaji: Hussein Javu, Hamisi Kizza, Mrisho Ngasa, Saimon Msuva, Jerson Tegete na Didier Kavumbagu.
Waati huo huo klabu ya Yanga imewasilisha barua ya malalamiko kwa TFF juu ya mchezaji Mohamed Hussein Neto kuchezea timu ya Mgambo JKT pasipokuwa na uhamisho wa kimataifa ITC, kibali cha kuishi na kufanya kazi nchini, mchezaji huyo ni raia wa Kongo na jina lake halisi ni Noel Melondoo.