VILABU VYA PREMIER LEAGUE VYAVUJA REKODI YA MAPATO - VYAINGIZA PAUNDI BILLIONI 2.36 KWA MWAKA

Vilabu vya Premier League ya England vimeweka rekodi ya kukusanya mapato yanayofikia kiasi cha £2,360m katika msimu wa 2011/12, kwa mujibu wa ripoti ya 22 ya masuala ya fedha kwenye soka kutoka Sports Business Group ya Deloitte.
kwa jumla, mapato ya vilabu 92 vya juu vya England yanazidi £3 billion kwa mara ya kwanza.
Dan Jones, Partner in the Sports Business Group kwenye kampuni ya Deloitte, alisema: "Pamoja na kuendesha shughuli zao kwenye mazingira magumu ya kiuchumi, vilabu vya Uingereza vinazidi kupata majina, kutambulika na kuzidi kuvutiwa watu wengi duniani mambo yanayopelekea mkusanyo mkubwa wa mapato yao.
"Mapato yote ya vilabu vya Premier League yameongezeka kwa asilimia  4% karibia kufikia £2.4 billion"

Karibia 75% ya mapato ya vilabu vya Premier League yaliongeka msimu wa 2011/12 yalitumika kwenye mishahara, ambayo ni ongezeko la £64m (4%) ya £1.7 billion ya mishahara ya yote vilabu vya Premier League.

Mapato kwenye  Football League Championship yameongezeka kwa zaidi ya £53m (13%) ya £476m msimu wa 2011/12.

0 maoni:

Post a Comment

 
Top