Iago Aspas anategemewa kukamilisha uhamisho wake kwenda Liverpool utakaogharimu kiasi cha £7.5million kutokea Celta Vigo baada ya leo mchana kuonekana akiwa nchini Uingereza tayari kwa kufanyiwa vipimo vya afya.
Aspas, 25, ambaye aliwasili England jana jumatatu, aliiambia Marca.com: "Nililazimika kukatisha mapumziko yangu huko Caribbean, ili kwenda England kukamilisha vipimo vya afya na Liverpool." Aspas anatajwa kuja kuziba pengo la Luis Suarez ambaye ametamka wazi kwamba anataka kuondoka huku akitoa ishara kwamba anataka kwenda Real Madrid baada ya leo kukaririwa akisema kwamba angependa kucheza timu moja na Cristiano Ronaldo.
|
0 maoni:
Post a Comment