WANASOKA WASOMI ZAIDI KWENYE ULIMWENGU WA SOKA DUNIANI - JUAN MATA, GLEN JOHNSON KIBOKO

1 SOCRATES

Gwiji huyu wa soka wa Brazil - alikuwa daktari kabisa lakini akachagua soka na kuachana na kuvaa koti jeupe.Socrates


2. MAROUANE CHAMAKH

Flop huyu wa ARSENAL pamoja na ubutu wake uwanjani lakini darasani alikuwa hatari - Chamakh ni mhasibu.


Marouane Chamakh

3 NEDUM ONUOHA


Kijana huyu anayekipiga kwenye timu ya QPR ni kichwa sana darasani. Onuoha aliwahi kupata a tatu kwenye masomo yake ya Hesabu, Biashara na Information Technology - Onuoah alifaulu vizuri mno kwenye masomo yake chuoni.
Nedum Onouha

4 SHAKA HISLOP

Mchezaji huyu wa zamani wa Newcastle ana degree ya mechanical engineering — na hata alikuwa anatumia muda wake wa mapumziko kufanya kazi NASA katika porject ya Space Station Freedom huko Washington. Raia huyu wa Trinidad Hislop alihusika katika project kubwa sana huko katika visiwa Caribbean.Shaka

5 JUAN MATA

Mchezaji huyu wa CHELSEA inawezekana ndio akawa mwanasoka mwenye elimu zaidi kuliko wote ndani ya kikosi cha Jose Mourinho - ana digrii mbili za Masoko na Sayansi ya Michezo.
Juan Mata

8 GLEN JOHNSON

Wanafunzi wenzie walikuwa wanamuita (HUMAN calculator) Glen Johnson anatumia masaa mawili kwa siku kwenda Chuo Kikuu Huria kuhudhuria masomo yake ya Degree ya Mahesabu. Glen Johnson

0 maoni:

Post a Comment

 
Top