CHELSEA YATHIBITISHA KUTUMA OFA YA KUMSAJILI WAYNE ROONEY - LAKINI YAKANUSHA KUTAKA KUWATOA AIDHA MATA AU LUIZ KWENYE DILI HILO

Masaa kadhaa baada ya kutoka kwa taarifa kwamba klabu ya Chelsea imetuma ofa ya paundi millioni 10 pamoja na mchezaji mmoja aidha David Luiz au Juan Mata kwa Manchester United ili kumsajili Wayne Rooney, sasa mabingwa hao wa Europ League wamethibitisha kutuma ofa kwa ajili ya kumsaini Rooney.

Lakini pamoja na kuthibitisha kutuma ofa hiyo, Chelsea wamekanusha taarifa kwamba ofa hiyo ilikuwa ni ya kiasi cha fedha pamoja kutoa mchezaji wao mmoja ili kuweza kumsaini Rooney.

Katika taarifa iliyotolewa na mtandao rasmi wa Chelsea - klabu imekiri kwamba jana usiku ilituma ofa kwenda United lakini haikuwa inahusisha mchezaji wao yoyote kuhusishwa na dili hilo.
  

0 maoni:

Post a Comment

 
Top