MADALA: JE GARETH BALE ANA THAMANI ZAIDI YA CRISTIANO RONALDO,MESSI NA NEYMAR?


Klabu ya Tottenham Hotspur ya England imegoma kumuuza winga wake Gareth Bale kwenda Real Madrid pamoja na kupewa ya uhamisho utakaoweza kuvunja rekodi ya dunia £82million. Inasemekana Spurs kupitia mwenyekiti wake Daniel Levy wanataka walipwe kiasi hicho cha pesa pamoja na wachezaji wawili wa Real Madrid Fabio Coentrao na Angel Di Maria ambao wote kwa pamoja wana thamani ya £45m, hivyo kufanya thamani ya dili la Bale kwa jumla kuwa £126 million ambazo ni fedha nyingi sana kuliko zile alizonunuliwa Cristiano Ronaldo kutoka Manchester United £80m.
Pia fedha hizo ni zaidi ya mara ya kiasi walicholipwa Santos na FC Barcelona - £51m kwa ajili ya kupata saini ya mchezaji bora wa mashindano ya Mabara Neymar.
Kubwa kuliko fedha wanayoitaka Tottenham ni nyingi kuliko ambayo ingeweza kumnunua mchezaji bora wa dunia Lionel Messi - ambaye kwenye mkataba wake na FC Barcelona kuna kipengele kinachosema ikiwa kuna klabu inayomtaka Messi basi inabidi ilipe kiasi cha Euro millioni 120 ambayo ni sawa na kama £100m. 

Je ni kweli Gareth Bale ana thamani kubwa kuliko Neymar, Cristiano Ronaldo na Lionel Messi? Kama Madrid wana uwezo wa kulipa fedha hizo nadhani bora wangeuvunja mkataba wa Lionel Messi. - Haya ni maoni yangu - je wewe mdau wa soka una maoni gani????????????????   

0 maoni:

Post a Comment

 
Top