Athletic Bilbao reject Manchester United's €30m bid for Ander Herrera

Inaonekana klabu ya Manchester United ina bahati mbaya katika soko la usajili la wakati huu baada ya leo hii ofa ya £30million kwenda Atheltic Bilbao kwa ajili ya kumsajili Ander Herrera kupigwa chini - huku Roma wakigoma hata kuanzisha mazungumzo juu ya usajili wa Daniele De Rossi. 

Kiungo mwenye miaka 24 wa kihispania, Herrera, aliwavutia United kwa muda mrefu sasa tangu Bilabo ilipowachakaza United katika Europa League misimu iliyopita.

Na De Rossi, 30, mshindi wa kombe la dunia ambaye ameshaichezea mechi 91 Italy na mmoja wa wachezaji wenye vipaji vikubwa na wanaolipwa fedha nyingi katikaSerie A.


Raisi wa Bilbao Jose Urrutia alikaririwa akisema kwenye mtandao wa Twitter: 'Kuna ofa imetumwa kwa ajili ya Ander Herrera. Tumeipokea jana na tumejibu kwamba hatuna mpango wa kuuza wachezaji wetu.
'Klabu yetu ni tofauti. Tunajenga mahusiano ya kihisia na wachezaji wetu. Kwetufedha sio jambo muhimu sana, ikitokea mchezaji anataka kuondoka basi inabidi aseme na klabu inayomtaka ilipe kiasi ambacho kimepangwa kwenye mkataba.'

Wakati huo huo Moyes ameshindwa kukanusha kwamba walituma kwa Herrera lakini akasema kamba ana matumaini ya kuongeza wachezaji kwenye kikos chake.
'Ninatumaini tutafanya baishara ya ununuzi kabla ya dirisha la usajili halijafungwa.'


0 maoni:

Post a Comment

 
Top