CHELSEA YACHAPWA 3–1 NA REALMADRID, RONALDO APIGA MAWILI
KIUNGO Frank Lampard alicheza kwa mara ya kwanza majira haya ya joto, lakini alishindwa kumzuia Cristiano Ronaldo kuinyanyasa Chelsea jana.
Kabla ya mechi hiyo na Real Madrid mjini Miami, kiungo huyo mkongwe alikosa mechi zote za kujiandaa na msimu za klabu, Stamford Bridge kutokana na kuwa majeruhi.
Lakini Lampard ameimarika na kuanza kazi tayari kwa mchezo wa kwanza wa Ligi Kuu dhidi ya Hull City, Agosti 18 baada ya kumaliza dakika 45 za kwanza katika Fainali ya Mabingwa wa Kimataifa wa Guinness.Katika mechi hiyo, mabao mawili ya Ronaldo na moja Marcelo, yalitosha kuitotesha timu ya Jose Mourinho 3-1 dhidi ya timu yake ya zamani ambayo kwa sasa inafundishwa na Carlo Ancelotii.
Chelsea ilipata bao lake pekee kupitia kwa Ramires.Mazungumzo baada ya tukio: Mourinho na kocha wa zamani wa Chelsea, ambaye kwa sasa ni kocha wa Madrid, Carlo Ancelotti wakizungumza baada ya mechiMapenzi yameisha: Shabiki la Real Madrid likiwa limebeba bango kuonyesha kutojali kuondoka kwa Mourinho katika klabu hiyoMabingwa: Nyota wa Real Madrid wakisherehekea kuifunga Chelsea katika fainali ya Mabingwa wa Kimataifa wa Guinness
Kikosi cha Real Madrid kilikuwa: Casillas, Arbeloa, Pepe, Ramos, Marcelo, Modric, Khedira, Isco, Ozil, Ronaldo na Benzema.
Chelsea: Cech, Ivanovic, Terry, Cahill, Cole, Lampard, Van Ginkel, Ramires, Oscar, Hazard na Lukaku.
0 maoni:
Post a Comment