Jose Mourinho amethibitisha kwamba Chelsea kwa sasa watasitisha mbio zao za kumuwania mshambuliaji wa Manchester United Wayne Rooney mpaka klabu hiyo itakapocheza na United kwenye dimba la Old Trafford siku ya jumatatu.

The Blues wameshuhudia ofa zao mbili zikikataliwa na mabingwa wa premier league, huku kocha David Moyes akisisitiza kwamba mshambuliaji huyo wa England hauzwi.
 

Jana jumatano zilitoka taarifa kwamba United wapo tayari kuzungumza na Chelsea katika dili la uhamisho wa Rooney lakini ikiwa tu litamhusisha Juan Mata - lakini Mourinho amesema hakuna mazungumzo yatakayofanyika mpaka baada ya mechi ya jumatatu.

"Tulituma ofa kwa ajili [Rooney] huko nyuma na tutfanya hivyo tena baadae," kocha huyo wa kireno aliwaambia waandishi wa habari baada ya ushindi wa 2-1 dhidi Aston Villa.

"Lakini sitaki Chelsea ifanye kitu chochote kabla ya mechi ya Jumatatu tutakapoenda Old Trafford."

0 maoni:

Post a Comment

 
Top