KUFURU: JAY Z AWAPA WAFANYAKAZI WAKE BONAS YA MILION 70 KILA MMOJA-MPAKA MFANYAKAZI WA NDANI
Hip hop mogul na mfanyabiashara mwenye ‘kisu’ cha maana (pesa) Shawn Carter a.k.a Jay Z licha ya kuwa baba mzuri kwa Blue Ivy, mume mzuri wa mkewe Beyonce lakini pia ni boss mzuri (tena sana) kwa wafanyakazi wake baada ya kuamua kuwapa ‘bonus’ ya kutisha (kwa ukubwa) ya mshahara.
Hivi karibuni Jay Z na Beyonce waliamua kurudisha fadhila kwa wafanyakazi hao wapatao 80 kwa kuamua kuwapa bonus ya zaidi ya $46,000 sawa na zaidi ya shilingi milioni 70 kila mmoja kutokana na kazi nzuri wanayoifanya.
Wafanyakazi waliodondokewa na zali hilo ambalo hawakulitegemea ni wale wa kampuni zake zote, club yake ya 40/40 hadi wale wafanyakazi wao wa nyumba zao 3 za Marekani.
Jay Z (43) aliamua kufanya wema huo baada ya kurejeshewa sehemu ya kodi ya ziada aliyolipa serikali ya Marekani ya $ 3.7sawa na zaidi ya shilingi bilioni 9 na kuona ni bora pesa hiyo arudishe fadhila kwa watu wanaomtumikia kwa bidii na uaminifu.
Kwa mujibu wa chanzo cha karibu na Jigga kiliiambia Daily star, hakuna aliyeachwa katika neema hiyo, na baadhi ya wafanyakazi hao walimpigia msaidizi wa Jay Z kumuuliza kama huenda wamepewa pesa kimakosa.
0 maoni:
Post a Comment