Lulu afanya shopping maalumu kwa ajili ya Uzinduzi wa filamu ya Foolish age kesho
Jana mchana mwanadada Elizabeth Michael alifanya shopping maalumu ya nguo na vitu vingine kwa ajili ya uzinduzi wa filamu yake mpya ya Foolish Age inayotarajiwa kuzinduliwa rasmi kesho kwenye ukumbi wa mlimani city jijini Dar es Salaam.
Uzinduzi wa filamu hii ambayo lulu mwenyewe anasema kuwa itakuwa ya kihistoria na aina yake utasindikizwa na wasanii mbalimbali wa kizazi kipya akiwema mwanadada Lady Jay dee.
Baada ya shopping hiyo mwanadada lulu pamoja na mama yake mzazi walipata nafasi ya kufanya mahojiano na kituo cha luninga cha DTV yote ni katika kuizungumzia filamu hii mpya inayotarajiwa kutingisha soko la filamu Tanzania

0 maoni:

Post a Comment

 
Top