MJADALA: ROONEY NA SUAREZ WATAENDELEA KUVICHEZEA VILABU VYAO SASA MSIMU UJAO? - JE ARSENAL NA CHELSEA NI MAHALA SAHIHI KWAO WOTE WAWILI?

Dirisha la usajili la barani ulaya linakaribia kufungwa mnamo September 2 mwaka huu. Timu kadhaa zimeshafanya usajili wa kuiimarisha vikosi vyao. Wachezaji wengi wameshahama kutoka kutoka timu moja mpaka nyingine. Lakini katika siku za hivi karibuni baada ya issue ya Gareth Bale kupoa - Luis Suarez na Wayne Rooney sasa ndio wanaongoza kutokea kwenye vichwa vya habari vya vyombo habari ulimwenguni.

Wayne Rooney anadaiwa kutaka kuondoka Manchester United na kujiunga na Chelsea ambao wameshatuma ofa mbili zilizokataliwa na United, lakini kocha Jose Mourinho amekaririwa akisema kwamba hatokata tamaa ya kumsajili mshambuliaji huyo mpaka siku ya mwisho ya usajili barani ulaya.

Luis Suarez yeye tofauti na Rooney - ameshathibitisha waziwazi kwamba anataka kuondoka Liverpool. Arsenal wameshatuma ofa ya £40m lakini Liverpool wameikataa kabisa huku wakisisitiza kwamba hauzwi. Kocha pamoja na mmiliki wa klabu hiyo wakisema Suarez hatoruhusiwa kuhama wakati huu kwa sababu bado wanamhitaji na hata kama wakimuuza watakosa mbadala wake hivyo kuidhoofisha timu yao. Kwa maana hiyo hawawezi kumuuza kwa bei yoyote.

Mjadala: Je Rooney na Suarez wataendelea kuvichezea vilabu vyao vya sasa au wataenda kujiunga na mahasimu wa vilabu?
Je ni Chelsea ni timu sahihi kwa Rooney? Au Rooney ataifaa Chelsea?
Luis Suarez anafanya uamuzi sahihi wa kutaka kuondoka Liverpool na kujiunga na Arsenal na je atasaidia?

0 maoni:

Post a Comment

 
Top