Serikali ya jamhuri ya muungano wa Tanzania kupitia mkuu wa mkoa wa Morogoro leo hii imemfanyia hafla fupi ya kumpongeza Bondia Francis Cheka aliyeiletea sifa kubwa nchi baada ya kushinda ubingwa wa dunia kwa kumtandika aliyekuwa bingwa wa dunia Phil Williams kutoka nchini Marekani.

Katika hafla hiyo fupi iliyofanyika katika viwanja vya Shujaa katika manisapaa ya Morgoro na kuhudhuriwa na mamia ya wakzi wa mji wa Morogoro wakiongozwa na mkuu wa mkoa Mh.Joel Bendera.

Akizungumza katika hafla hiyo Bendera alisema serikali imefurahishwa sana na ushindi wa Cheka ambao umeiletea nchi sifa kubwa katika anga ya kimataifa ya mchezo wa ngumi. Kutokana na jambo hilo serikali imeamua kumzawadia Francis Cheka kiwanja kikubwa, mabati ya nyumba nzima, mifuko 80 thamanini ya saruji na pia usimamizi na taratibu zote mpaka nyumba ya kisasa itakapokamilika kwa ajili kukabidhiwa kwa Cheka.

0 maoni:

Post a Comment

 
Top