Cesc Fabregas amekiri kwamba asingeweza kujiunga na  Manchester United wakati huu wa dirisha la usajili hata kama  David Moyes angemuongeza mshahara mara 3 wa anaopata sasa hivi ndani ya FC Barcelona.

United walikuwa wakimtaka kwa udi na uvumba nahodha huyu wa zamani wa Arsenal kwa kipindi kirefu cha msimu wa usajili huku ofa zao za £30million na £35m zikikataliwa.
Lakini Fabregas anasisitiza kwamba ahkutaka kabisa kuondoka nchini katika klabu yake ya utotoni.

Fabregas aliiambia The Sun: 'Ninsingeweza kuhama kwa fedha mara mbili au tatu ya mshahara wangu wa sasa.
'Nimelipa fedha zangu mwenye kuweza kucheza Barcelona. Nilikuwa nalipwa vizuri nikiwa Arsenal zaidi ya hapa. Kuna ndoto na hii ilikuwa ndio ya kwangu.
'United hawakuwahi kuongea nami. Klabu inapokutaka kawaida huongea na klabu na sio lazima iongee na mchezaji husika.

'Nilishasema siku zote kwamba sikuwa nimeongea na mtu yoyote - na kitu pekee nilichokuwa nikifikiria ni kufanikiwa nikiwa  Barcelona.
'Ukweli ni kwamba United walituma ofa rasmi kadhaa na hilo likaja kujulikana kabisa.
'Najua kuna sehemu nyingine ambapo wanatoa fedha nyingi, lakini hakuna muda niliwahi kufikiria kuondoka hapa.'

0 maoni:

Post a Comment

 
Top