Na Dustan Shekidele, Morogoro
MASKINI Daz Baba! Ndivyo unavyoweza kusema kufuatia habari ya kusikitisha ya msanii huyo ambaye jina lake kamili ni David Jacob kunaswa akiwa amezima mjini hapa huku ulevi wa kupindukia ukidaiwa kuwa chanzo.
Daz Baba au Daz Mwalimu asubuhi ya Agosti 5, mwaka huu alinaswa na kamera za gazeti hili akiwa hajitambui kwenye eneo maarufu kwa jina la Itigi lililopo nje ya Stendi ya Mabasi ya Msamvu ikidaiwa kuwa alifika mitaa hiyo tangu usiku wa jana yake.

Awali chanzo chetu cha habari kilitupigia simu na kutueleza juu ya kuzimika kwa msanii huyo aliyekuwa akiunda Kundi la Daz Nundaz Family na baada ya paparazi wetu kufika eneo la tukio ambalo ni maarufu kwa biashara haramu ya ukahaba, lilibaini kuwa ni yeye na wasamaria wema walikuwa wakijaribu kumuamsha bila mafanikio.
“Huyu atakuwa amelewa sana na inawezekana katumia madawa ya kulevya au kawekewa madawa kwenye bia. Dah! Inasikitisha sana kwa msanii kama huyu ambaye huko nyuma alikuwa aking’ara kwenye anga la muziki,” alisikika akisema kijana mmoja aliyekuwa eneo hilo.
Hata hivyo, jitihada za kumuamsha ziligonga ukuta na mpaka paparazi wetu anaondoka eneo la tukio bado msanii huyo alikuwa hajitambui na mfukoni hakuwa na kitu, ikiashiria kuwa wahuni walimkomba kila kitu

0 maoni:

Post a Comment

 
Top