Roberto Carlos amewaonya Chelsea kwamba mshambuliaji wao mpya Samuel Eto'o anaweza kawa na ushawishi mbaya ndani ya chumba cha kubadilishia nguo.

Mkurugenzi huyo wa zamani wa timu ya Anzhi Makhachkala amesema kwamba mshambuliaji huyo mcameroon aliingilia majukumu yake ya kazi wakiwa pamoja katika klabu hiyo ya Russia mpaka kufikia hatua kwamba alianza kufikiria kujiuzulu.
Mwaka 2011, Carlos alikuwa Anzhi wakati timu hiyo ilipomnunua Eto'o kutoka Inter Milan, na kumfanya mchezaji huyo kuwa mwanasoka anayelipwa fedha nyingi zaidi duniani. 


Baada ya kufunga mabao 36 katika mechi 71 akiwa na Anzhi, Eto'o amehamia Chelsea kwa uhamisho huru na anaweza kuanza katika mechi yake ya kwanza dhidi ya Everton jumamosi hii.

Lakini mahojiano na gazeti la Globo, Carlos ameelezea na namna Eto'o alivyomfanyia wakati wakiwa Anzhi.
Alisema: 'Nimemfahamu Eto'o tangu nikiwa na miaka 16, na kutokea wakati huo amekuwa mtu mzuri kwangu niliyempenda. 
'Ni mtu mzuri, lakini kuna kitu kuhusu yeye 'ubinafsi' ndio kinachoharibu sifa yake. 
'Wakati mchezaji ambaye badala ya kucheza vizuri - hukaa na kujariu kulazimisha kusajiliwa kwa wachezaji ambao ni marafiki zake - ni suala la kusikitisha na linachanganya na kushangaza hasa kwa mchezaji kama Eto'o. Alifanya yote haya akiwa Anzhi lakini sio kucheza soka la kiwango kikubwa.'



Akizungumiza namna mahusiano yao yalivyoharibika, Carlos alisema: 'Nilienda kwenye klabu na katika mwaka wangu wa kwanza timu ilimaliza kwenye nafasi tano za juu.
'Tuliweza kuiweka timu kuwa katika ueledi wa 100%. Mwaka wa pili, tukamsaini Eto'o na nilikuwa na control ya timu - Nilifanya kazi na wachezaji na makocha. Nilifanya kazi nzuri katika kuifanya Anzhi kuwa miongoni mwa timu bora.

'Kuwasili kwa Eto'o, huku thamani ya kila ikijulikana, nilipata matatizo kidogo katika chumba cha kubadilishia nguo na ikabidi niongee na wachezaji wa kirusi na kuwaelezea kwanini Eto'o alikuwa pale. 
'Japokuwa, ukafika wakati Eto'o akaanza kuingilia majukumu yangu, kutaka kuwa na mamlaka ndani ya timu, majukumu yangu na yale ya kocha Guus [Hiddink].

'Tuliongea kuhusu jambo moja, na baada hapo alikuwa anaenda kwa wachezaji anawaambia jambo lingine. Hilo lilinikera sana na nilionya ningeondoka.
'Hakuna aliyeniamini kwa sababu nilikuwa na mkataba wa miaka minne. Lakini baadae niliwaita Anzhi na kufikia makubaliano.'
Carlos, 40, tangu wakati akaondoka na sasa anafanya kazi kama mkurugenzi wa timu Sivasspor huko Turkey. Mmiliki wa Anzhi Suleyman Kerimov aliamua kuondokana na matumizi makubwa ya klabu na kupelekea kuuzwa kwa wachezaji kadhaa.

0 maoni:

Post a Comment

 
Top