Kampuni ya GS1 (TZ) National Limited iliyoko Msasani karibu na hospitali ya CCBRT, leo hii imemkabidhi Rapper Professor Jay Barcode itakayokuwa ikitumika katika kazi zake za muziki na kumuwezesha
kuuza kazi zake online na hata kuingia katika chart kubwa duniani kama Billboard na zinginezo na kumfanya aweze kutanua soko la kazi zake duniani kote.




GSI imeanzishwa kwa kusudio kubwa la kuweza kutoa huduma za Barcodes na teknologia nyingine zinazotewa na taasisi GS1 ulimwenguni, za kuendeleza biashara kimataifa na kitaifa. 

Imedhibitika kwamba chombo hiki, kabla ya kusajiliwa nchini,  wafanyabiashara wengi wa Tanzania walikuwa wakizifuata huduma za barcodes kutoka nchi za Kenya na Afrika ya Kusini. Chombo hiki kinasimamiwa na Mkutano Mkuu wa mwaka na Bodi ya Wakurugenzi.

0 maoni:

Post a Comment

 
Top