Klabu ya Ahly ya Egypt imeshinda taji la nane la klabu bingwa Barani Afrika baada ya kuifunga  Orlando Pirates  ya Afrika Kusini mabao 2-0 kwenye mchezo wa fainali uliopigwa leo jijini Cairo.

Ahly, waliokuwa mabingwa watetezi wameshinda kwa jumla ya mabao 3-1 baada ya mchezo wa kwanza uliopigwa nchini Afrika Kusini kumalizika kwa sare ya 1-1.
Mshambuliaji mkongwe Mohamed Aboutrika aliipatia Ahly bao la kuongoza mnamo dakika ya 54 kabla ya Ahmed Abdul Zaher hajaitimisha ushindi pale alipofunga bao la pili kunako dakika 78 kwa shuti lilimshinda kipa wa Pirates Senzo Meyiwa.

0 maoni:

Post a Comment

 
Top