Jose Mourinho amesema kwamba kumfundisha Cristiano Ronaldo walipokuwa Real Madrid kinabakia kuwa kitu muhimu na kizuri katika maisha yake.
Wawili hao walikaa pamoja kwa miaka mitatu ndani ya Santiago Bernabeu, huku Ronaldo akifunga jumla ya mabao 168 katika mechi 164 wakati Mourinho akiwa katika benchi la Bernabeu.
Na japokuwa imewahi kuripotiwa kwamba hawakuwa wakielewana walipokuwa Madrid, lakini kocha wa sasa wa Chelsea amemsifia sana mshambuliaji huyo mwenye miaka 28.
"Kumfundisha Ronaldo kilikuwa kitu kikubwa sana kwenye maisha yangu ya ufundishaji," Mourinho aliiambia France Football.
"Ndio mchezaji mweledi zaidi ambaye nimewahai kumuona.
"Kocha na mchezaji wanaweza kuwa na tofauti zao kwa muda fulani, lakini inashiia pale pale, sina tatizo nae.
"Kuwa na Ronaldo katika klabu moja ni kitu bora kabisa kilichowahi kunitokea kwenye soka. "
Ronaldo mpaka sasa ameshafunga mabao 24 katika mechi 17 alizocheza msimu huu katika mashindano yote, na jana usiku aliingiza mguu mmoja timu ya Ureno katika mashindano ya kombe la dunia baada ya kuifunga Sweden 1-0 katika mechi ya kufuzu kucheza World Cup 2014.
0 maoni:
Post a Comment