Goli la mdachi huyu liliamua mechi ya hivi karibuni baina ya Man United na Arsenal, lakini Je Mashetani Wekundu wamekuwa wakimtegemea zaidi Robin van Persie kwenye ufungaji?

Mwaka mmoja uliopita, niliandika makala fupi kuhusu mwanzo m'baya wa Arsenal katika msimu wa
 2012/13, wakiwa na safu butu ya ushambuliaji huku wakiwa wametoka kumpoteza Robin van Persie. Wakati huo Arsenal walikuwa wanahangaika sana kufunga mabao huku mabao ya Van Persie yakiwa tayari yamempa uongozi katika listi ya ufungaji huku Man United wakiwa nyuma kwa pointi moja kutoka kwenye timu iliyokuwa ikiongoza ligi. Ulikuwa ni ushahidi tosha kwamba Arsenal walikuwa wakimtegemea mno mholanzi huyo katika msimu wa nyuma wa 2011/12 , na bado wakati huo pia walishindwa kushindana na safu ya ushambuliaji iliyoundwa Rooney, Hernández, Welbeck, kwa idadi ya mabao.

Mwaka mmoja mbele, hali inaonekana kubadilika. Kama chati inavyoonesha hapo chini, baada ya michezo 11 msimu wa EPL, United imefunga jumla ya mabao 18, saba yakiwa yamefungwa na Van Persie. Ukiondoa mabao hayo saba katika 18, timu ingekuwa na rekodi ya tano kwa ubovu katika upachikaji mabao katika ligi.. 

Kwa utofauti upande wa Arsenal, ukitoa magoli sita yaliyofungwa na mchezaji anayeongoza Aaron Ramsey, kutoka katika jumla ya mabao yao 22, Gunners bado wangekuwa na rekodi nzuri ya ufungaji wa mabao katika ligi. Mabao ya hivi karibuni ya Van Persie dhidi ya Arsenal, Stoke, na Southampton, yanamaanisha kwamba United imeshinda mechi mbili na kutoa suluhu mara 1, badala ya kutoa suluhu mara mbili na kupoteza mechi moja. Bila mabao ya Van Persie - Pointi tano walizopata United wangejikuta kwenye nafasi ya tisa. Arsenal, hata bila ya pointi nne walizopata kwa mabao ya Ramsey dhidi ya Sunderland na Swansea, bado wangeweza kuwemo katika Top 4. 
Japokuwa msimu uliopita United iliweka rekodi ya kuwa na wafungaji wa mabao 20 tofauti, lakini msimu huu mpaka sasa ni wachezaji sita tu tofauti waliofunga magoli ya United katika EPL tangu mwezi August. Kama ambavyo unaona kwenye chati hapo juu, Arsenal tayari wana wafungaji 10 tofauti wa mabao msimu huu mpaka sasa.

Hii inanipa ishara kwamba Arsenal ndio wana kikosi kilicho na uwiano mzuri. Timu inaonekana kutowategemea sana wafungaji  Ramsey na Olivier Giroud kuliko United wanavyotegemea mabao ya RVP na Rooney. Hata Liverpool, ambao wana tofauti ndogo ya mabao nyuma ya Arsenal, wana utegemezi mkubwa wa mabao ya  Luis Suárez na Daniel Sturridge, ambao wamefunga mabao 16 kati ya 20.

Mashabiki wengi wamekuwa wakitoa maoni yao kwamba tofauti na United pamoja Liverpool, ambao wana bahati ya kuwa safu za ushambuliaji zinazoundwa na Suarez/Sturidge na Rooney/RVP, Arsenal wanamtegemea zaidi Giroud kwa mabao yao. Lakini bado washambuliaji wengine wa Arsenal wameonyesha wana uwezo kumsapoti mshambuliaji huyo wa kifaransa, wakifunga mabao 15 mengine. Idadi hii haijafikia hata na kundi zima la viungo wa Chelsea.

Pamoja na kuwa na wafungaji tofauti msimu uliopita, kiungo pekee wa United ambaye alichangia mabao mengi alikuwa Shinji Kagawa na mabao sita. Na mabadiliko pekee yaliyofanyika kwenye safu hiyo ni kuondoka kwa Paul Scholes na kuja kwa Maroune Fellaini, ambaye abado ameshindwa kuwa na kiwango alichokuwa nacho msimu uliopita na Everton ambapo alifanikiwa kufunga mabao 11.


Kuna habari nzuri kwa Arsenal kwamba wamekuwa wakicheza karibia msimu mzima bila washambuliaji tegemeo ambao walikuwa kwenye top 3 ya wafungaji bora msimu uliopita kwenye timu yao, Theo Walcott na Lukas Podolski. Kurejea kwa washambuliaji hawa wawili kutamuongezea machaguo Wenger katika kukiongezea makali kikosi chake.

Liverpool na United wanaweza kuwa na washambuliaji wazuri zaidi kwenye ligi, lakini bado ni Arsenal wanaonekana kuwa na safu kali zaidi kwenye msimu huu. Van Persie na Rooney walionyesha ubora wao wakati timu hizi mbili zilipokutana wiki kadhaa zilizopita, lakini endapo majeruhi wa Arsenal watakaporejea, kikosi cha Arsenal kitakuwa vizuri zaidi. Ikiwa watasajili mshambuliaji mwezi January itakuwa bora zaidi kwa Gunners. Ni United ambao wanategemea zaidi mabao ya Van Persie msimu huu, na ni Arsenal wenye kikosi cha makali zaidi msimu huu. 

*TAKWIMU ZA MAKALA HII HAZIHUSISHA MECHI ZA WIKIENDI HII NA ILIYOPITA*
 
Top