Na Baraka Mpenja, Dar es salaam
WAPENZI
wa soka nchini wameombwa kujitokeza kwa wingi kuomba kadi za uanachama
katika klabu ya Ashanti United yenye makazi yake maeneo ya Ilala, jijini
Dar es salaam.
Afisa
habari wa Ashanti, Marijani Rajab ameuambia mtandao huu kuwa mwenye nia
ya kujiunga na timu hiyo ya wananchi au ya kijamii afike ofisi zao
zilizopo maeneo ya Ilala.
“Tupo
Ilala, ofisi zetu zinatazamana na jengo la Mwalimu House, ni jengo dogo
na chini yake kuna ofisi za DAWASCO au fika Ilala sokoni kwa wauza
mitumba, muulize mtu yeyote ofisi za Ashanti, bila shaka atakuonesha, ni
rahisi sana”. Alisema Marijan.
Marijan
aliongeza kuwa katika kadi zao wanatumia picha za kidijitali ambazo
wanapiga wao na gharama ya picha hizo ikiwa ni pamoja na ada ya awali
ya kadi hiyo ni shilingi za Kitanzania elfu kumi na moja tu (11,000/=)
na baada ya dakika kumi kadi yenye ubora wa juu inatolewa.
“Kadi
zetu ni za kisasa zaidi, karibuni wote wanaotaka mapinduzi ya soka la
Tanzania. Njoo uungane na watanzania wenzako wenye mapenzi na Ashanti
Unted. Timu hii ni ya Kihistoria, ina malengo makubwa ya kufuta ufalme
wa Simba na Yanga”. Alisema Marijan.
Afisa
habari huyo alifafanua kuwa kama kuna mtu anataka kujiunga na matawi,
Ashanti wana tawi kubwa linaloitwa Napoli na mtu yeyote anaweza kwenda
hapo kumuuliza katibu kuhusu taratibu zao ambazo ni rahisi sana.
Marijan
aliwatoa hofu watu kuwa vigezo na masharti ni vilevile kwa mujibu wa
sheria, mtu awe na umri wa miaka 18, awe na akili timamu na vingine
ambavyo sheria na katiba inaruhusu.
Aliongeza kwa kutoa wito kwa watanzania kujiunga na timu hii ya kijamii ili kutoa `Ubepari` wa Simba na Yanga.
“Timu
zinazoonekana kuwa na mwelekeo wa kuondoa ufalme wa Simba na Yanga ni
zile za makampuni binafsi. Lakini Ashanti ni timu ya kijamii, ina
uhusiano mkubwa na wananchi. Ina malengo ya kuuondoa Ukurwa na Udoto wa
Simba na Yanga”.