Muigizaji nyota, Lesego Motsepe, ambae alikuwa akijulikana kama Letti Matabanne katika tamthilia ya Isidingo amefariki dunia.
statement iliyotolewa kwa niaba ya familia ya Motsepe inasema kuwa, alikutwa akiwa ameshafariki na kaka yake "Moemise Motsepe" akiwa nyumbani kwake mida ya saa tano asubuhi,

Mwaka 2011, siku ya ukimwi duniani, Motsepe alijitangaza hadharani hali yake ya VVU katika kusaidia kupambana na unyanyappaa dhidi ya watu wanaoishi na ugonjwa huo. Alifanya pia warsha kadhaa na mazungumzo juu ya umuhimu wa kuishi kwa matumaini  kwa walioathirika na Ukimwi moja kwa moja au vinginevyo. Yeye pia alifanya kazi kama balozi wa Ukimwi kwa miaka mingi, kuwaelimisha watoto katika jamii mbalimbali.
 
Top