Meneja wa klabu ya Arsenal, Arsene Wenger amethibitisha kwamba hatua za kinidhamu zitachukuliwa dhidi ya Olivier Giroud baada ya mshambuliaji huyo kukiri na kuomba msamaha kwa kumuingiza mwanamke kwenye chumba cha hoteli waliyokuwa wameweka kambi kabla ya mchezo wa Crystal Palace.

Giroud ambaye ni mume wa mtu mwanzoni alikataa kabisa kumuingiza mwanamke Celia Kay katika chumba cha hoteli cha Four Seasons Hotel huko Canary Wharf usiku wa kuamkia kwenye mechi ya ushindi wa 2-0 dhidi ya Crystal Palace February 2 mwaka huu. Lakini jana usiku Giroud aliomba msamaha kwa mkewe na kocha wa Arsenal baada ya gazeti la Sunday Sun kuchapisha picha za Giroud akiwa ndani ya nguo ya ndani na mwanamke.
Wenger alisema: ‘Ni suala la ndani na nisingependa kuliongelea sana kwa sababu ni suala linalohusu maisha yake binafsi."

Picha mabyo imesambaa ilipigwa na mwanamitindo ambaye alilala na Giroud kwenye chumba cha hoteli waliyofikia Arsenal.

Giroud alitumia mtandao wa Twitter na kuomba msamaha kwa mkewe Jennifer - ambaye ametoka kumzalia mtoto wa kiume mshambuliaji huyo miezi sita iliyopita, pia aliomba msamaha kwa klabu yake. 
   

‘Naomba radhi kwa mke wangu, familia na marafiki zangu, pia kocha na wachezaji wenzangu pamoja na mashabiki wa Arsenal," alisema.

‘Sasa nina jukumu la kupigania familia na timu yangu ili niweze kupata msamaha wao. Hakuna kingine chenye umuhimu zaidi hili hivi sasa.' 
Mwanamitindo Kay
Mwanamitindo Kay, ambaye hufanya kazi na majarida ya kimataifa kama Maxim na FHM, alipigwa picha akiwasili katika hotel ya Four Seasons huko Canary Wharf saa 12.50am na kuondoka saa 3.04am usiku huo huo.
Hata hivyo Kay amesisitiza hakufanya mapenzi na mshambuliaji huyo, ambaye alikwepa faini kutoka kwa klabu yake baada ya kumwambia Wenger kwamba hakukutana na mwanamke huyo usiku huo.

‘Olivier anajua ukweli na suala la kuongopa kuhusu suala letu ni upumbavu,' Kay aliliambia gazeti la Sun on Sunday.

‘Anajichimbia shimo kubwa mwenyewe. Kama aliweza kutenda kosa basi akiri makosa na atumikie adhabu zake.' 
Inaaminika Arsenal watampiga faini ya £230,000. 
 
Top