Na Baraka Mbolembole
Brazil iliifunga Croatia katika mchezo wa kwanza wa hatua ya makundi, Juni 13, mjini Berlin kwa bao 1-0. Timu hizo zitakutana tena baada ya kupita kwa miaka nane katika mchezo wa ufunguzi wa michuano ya ijayo ya kombe la dunia, Juni 12, mwaka huu katika uwanja wa Arena de Sao Paulo.

Mambo mengi yamebadilika tangu wakati ule kiungo mshambuliaji, Ricardo Kaka' alipoifungia, Selecao pekee katika mchezo wa mwisho kati ya timu hizo mbili. Croatia, chini ya kocha Niko Kovac, na wasaidizi wake, Robert Kovac ( mdogo wake Niko), Goran Lackovic na Vatroslav Miliacic, inasotea ushindi wake wa kwanza katika michuano tangu walipoifunga
Italia mabao 2-1, juni 8, 2002.
 
CROATIA
 Croatia ilishindwa kufuzu katika fainali zilizopita nchini Afrika
Kusini, washindi hao wa tatu wa mwaka 1998, wanarekodi ya kushinda michezo saba kati ya 13 waliyocheza katika fainali tatu walizofuzu miaka ya nyuma, huku ushindi wao mkubwa ni ule dhidi ya Ujerumani, Julai 4, 1998 walipoifunga kwa mabao 3-0 katika mchezo wa robo fainali. Mechi yao ya kukata utepe dhidi ya Brazil inatarajiwa kuwa kali kwa kuwa nchi hiyo inao wachezaji wa viwango vya juu kwa sasa barani Ulaya.

CAMEROON INAWEZA KUVUKA KUNDI HILI
Katika mchezo mwingine wa kundi A, timu za Mexico na Cameroon, zitapambana juni 13, katika uwanja wa . Pengine ni timu iliyofuzu kwa utata mkubwa kuliko nchini nyingine yoyote. Cameroon ilimaliza nyuma ya Libya katika harakati za kufuzu kwa hatua ya mtoano katika kundi,' Simba wasiofugika' walipata nafasi ya kuikabili Tunisia na kuitupa nje na kufuzu kwa fainali za Brazil.

Ingawa hawana matokeo mazuri tangu mwaka 90, Cameroon si  timu ya kudharauliwa kwa namna yoyote. Kwa upande wa Mexico, timu hiyo ya Amerika ya Kati, iliishia katika hatua ya mtoano mwaka 2010 walipoondolewa na Argentina.  Mafanikio yao makubwa katika michuano hiyo ni yale ya miaka ya 1970, na 1986 walipoishia hatua ya robo fainali. Watacheza na Brazil, juni 17 na kumaliza na Croatia, Juni 23 ikiwa ni marudiano ya mpambano wao wa mwaka 2002 katika fainali za Korea kusini na Japan. Mexico ilishinda 2-1.

NYEPESI NYEPESI
Brazil inashikilia rekodi ya kucheza fainali mara tatu mfululizo. Walifanya hivyo katika miaka ya 1994, walipoifunga Italia kwa changamoto ya mikwaju ya penati, katika fainali za Marekani. Wakapoteza kwa mabao 3-0, dhidi ya waliokuwa wenyeji Ufaransa, 1998, na wakatwaa tena taji mbele ya Ujerumani, 2002, kwa ushindi wa mabao 2-0 katika fainali za Korea Kusini na Japan.

UJERUMANI
 ndiyo timu iliyopoteza michezo mingi ya fainali za kombe la dunia. Imepoteza mara nne, 1966 dhidi ya waliokuwa wenyeji England, 1982 dhidi ya Italia, katika michuano ilipigwa nchini Hispania, wakalala tena mbele ya Argentina katika fainali za Mexico, 1986, na mara ya mwisho walilala dhidi ya Brazil, 2002.

Roger Millar aliisaidia timu ya Cameroon kufika robo fainali mwaka 1990 na kutolewa na England kwa kufungwa mabao 3-2 katika muda wa ziada. Mshambuliaji huyo wa zamani wa Cameroon alikuwa na miaka 42 na siku 39 wakati alipoiwakilisha Cameroon dhidi ya Urusi, Juni 28, 1994 katika fainali zilizofanyika nchini Marekani.
 
Top