Ronaldo beats Messi to top Goal Rich List

Kwa mujibu wa mtandao wa Goal.com, nahodha wa timu ya taifa ya Ureno na mwanasoka bora wa dunia Cristiano Ronaldo ndio mwanasoka tajiri zaidi duniani.

Katika listi hiyo iliyotangazwa leo, Ronaldo amerithi nafasi ya kwanza iliyokuwa ikishikiliwa na David Beckham kwa muda mrefu kaba ya kustaafu msimu uliopita. Ronaldo ambaye alisaini mkataba mnono zaidi na Real Madrid miezi kadhaa iliyopita amempita mshindani wake Lionel Messi na mwanasoka anayelipwa zaidi kimshahara Wayne Rooney.

Samuel Eto'o ndio muafrika pekee aliyeweza kuingia kwenye listi ya wanasoka matajiri zaidi duniani.

LISTI KAMILI
1. Cristiano Ronaldo £122m
2. Lionel Messi £120.5m
3. Samuel Eto'o £70m
4. Wayne Rooney £69m
5. Kaka £67.5m
6. The Neymar family £66m
7. Ronaldinho £64m
8. Zlatan Ibrahimovic £57m
9. Gianluigi Buffon £52m
10. Thierry Henry £47m
SOURCE: Goal.com
 
Top