Who has been the better signing - Gareth Bale or Neymar?
Usajili wao katika vilabu vya Real Madrid na FC Barcelona wakati wa dirisha 
kubwa la usajili lilopita ndio ulitingisha zaidi vyombo vya habari duniani - Neymar alijiunga FC Barcelona na Gareth Bale alienda Real Madrid.

Wakati tukielekea kushuhudia El Classico wikiendi hii, ebu tutazame nani kati yao hawa wachezaji wawili amekuwa ndio usajili mzuri ndani ya vilabu hivi vikubwa duniani.

Bale alianza msimu kwa wakati mgumu sana kwa kuwa na majeruhi ya mara kwa mara, Neymar alianza vizuri ingawa nae hapa katikati alipata majeruhi kwa wiki kadhaa ila amerudi.

Katika mechi ya kwanza ya El Classico Neymar alitoka anacheka, Bale na timu yake walitoka kwenye dimba la Camp Nou baada ya kufungwa. Real Madrid wakiwa kileleni kwa tofauti ya pointi 4 - mechi ya wikiendi dhidi ya FC Barcelona inaweza kuamua bingwa wa La Liga msimu huu.

Tukielekea kwenye mchezo huo ni vizuri tutazame nani baina ya Gareth Bale na Neymar - wachezaji wenye umri mdogo waliosajiliwa kwa fedha nyingi - yupi kati yao amekuwa bora zaidi ya mwenzake katika msimu wao wa kwanza ndani ya vilabu vyao.

Kitakwimu Gareth Bale amemzidi Neymar. Bale amefunga mabao 14 katika mechi 27, yakiwemo manne katika Champions League. Neymar amefunga mabao 10 katika mechi 28, matatu katika Champions League. Pia Bale ameshatoa pasi za 

magoli 14 wakati Neymar amefanikiwa kutoa 11.

Baadhi wanaweza kusema takwimu zinaweza zisitoe uhalisia wa mambo, lakini namba hazidanganyi na kwenye hili unaweza kabisa kuona kwamba Bale amekuwa usajili zaidi kuliko Neymar.

Wakati Neymar amekuwa akihangaika kuunda safu nzuri ya mashambulizi na Messi, Bale amekuwa mwiba mchungu kwa timu pinzani akiisaidia Madrid kukamata kilele cha La Liga kwa ushirikiano mzuri alionao na Ronaldo pamoja na Karim Benzema.



 
Top