Mshambuliaji Lionel Messi jana alivunja rekodi na kuweka rekodi mpya ndani ya klabu ya FC Barcelona baada ya kufunga mabao matatu katika mchezo wa ushindi wa mabao 7-0 dhidi ya Osasuna.
Messi kwanza alimfikia Paulinho Alcantara kwa kufikisha mabao 369, rekodi ambayo imekaa kwa takribani miaka 80, Paulinho alifunga mabao 142 katika mechi za mashindano - 227 katika mechi za kirafiki. Aliichezea Barca kutoka 1912 mpaka 1927, hata Alcantara aliumia na hakucheza misimu miwili katika kipindi chote.
Messi baada ya kuifikia rekodi hiyo, akaongeza mabao mawili na kuweka rekodi mpya ya kuwa mfungaji bora wa muda wote wa klabu hiyo katika mechi zote akifikisha mabao 371 - mabao 344 amefunga katika mechi za mashindano, 27 katika mechi za kirafiki.