Msanii na msemaji mkuu wa Weusi Nikki wa Pili, ametoa tamko juu ya msanii mwenzao Lord Eyes na kusema kuwa kampuni kama kampuni imemsimamisha Lord Eyes na kwa yeyote anaetaka kujua habari zake amtafute Lord mwenyewe.
"Tamko ni kwamba Lord Eyes amemsimamishwa kazi, kampuni imemsimisha kazi, kwahiyo kuanzia sasahivi habari zote za Lord Eyes ataziripoti Lord Eyes mwenyew, sababu za kumsimamisha ni za ndani ya kampuni kwahiyo hatuwezi kuzitoa. Kampuni yoyote inamisingi yake ambayo inafanya maamuzi.kwa mamlaka ya kampuni hatuwezi tena kumzungumzia Lord Eyes, kwasasa hivi yeye sio member wa Weusi amesimamishwa mpaka hapo tutakapotangaza upya kumrudisha. Kwahiyo taarifa za Lord Eyes ni zake sio za Weusi tena" amesema Nikki wa Pili
 
Top