Mwanasoka gwiji wa Nigeria Nwankwo Kanu amefanyiwa upasuaji wa moyo huko nchini Marekani katika hosptali ya Cleveland Hospital iliyopo Ohio, hospitali ambayo pia ilimfanyia upasuaji wa kwanza mnamo mwaka 1997, alipoanza kusumbulia na matatizo ya moyo. 

Mratibu wa Kanu Heart Foundation, Onyebuchi Abia, amethibisha kwamba upasuaji huo umekuwa na mafanikio na kwamba mshambuliaji huyo wa zamani wa Arsenal na Inter Milan ameshatolewa katika chumba cha uangalizi maalum na tayari ameanza kupata nafuu taratibu. 
"Atarudi nyumbani katika siku chache zijazo, niliongea jana jumapili jioni na amenithibitishia  kwamba yupo kwenye hali nzuri." Abia alisema kwenye taarifa iliyotolewa.
 
Top