Gazeti la kihispania AS linaripoti kwamba mwanasoka tajiri zaidi na bora Cristiano Ronaldo anayekipiga katika klabu ya Real Madrid ameamua kumlipia fedha za matibabu mtoto mwenye miezi 10 Erik Ortiz Cruz ambaye ni mgonjwa sana akisumbulia na matatizo kwenye ubongo wake (Cortical dysplasia.)
Ugonjwa huu unamfanya mtoto huyo awe anazimia au kupata mshtuko mara 30 kwa siku na hivyo anahitaji kufanyiwa upasuaji ili kuondoa hali hiyo isiyo ya kawaida kwenye ubongo. (Kufahamu zaidi kuhusu cortical dysplasia ingia hapathe Wikipedia entry here.)
Kila kipimo anachofanyiwa mtoto huyo kina gharama ya 6,000 euros na upasuaji mzima unagharimu kiasi cha 60,000 euros hivyo watu wa kijiji cha Villaluenga de la Sagra, Spain, wamekuwa wakijaribu kukusanya fedha kwa ajili ya matibabu ya mtoto huyo kupitia michango.
Jambo hili lilipomfikia Ronaldo ambaye alifuata aweze kutoa jezi yake na viatu vyake ili vipigwe mnada, akawapa walichotaka kwa ajili ya mnada na kisha akalipia gharama zote za matibabu ya mtoto huyo.
Hii si mara ya kwanza kwa Ronaldo kusaidia watu wasiojiweza, kitendo hiki kinakuja siku chache baada ya kutajwa kuwa manasoka tajiri zaidi duniani.