Wachezaji wa Young Africans Sports Club
Bao la dakika ya 82 ya mchezo liliowekwa wavuni na Naodha wa timu ya Young Africans Nadir Haroub "Cannavaro" limepelekea watoto wa Jangwani kuvunja mwiko wa Waarabu baada ya dakika 90 za mchezo za mwamuzi Bezez Haileysus kumalizika na kuibuka na ushindi wa bao 1-0 mchezo uliofanyika dimba la Uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam.
Young Africans ambayo tangu ianze kushiriki  mashindano ya Klabu Bingwa Barani Afrika ilikuwa haijawahi kupata ushindi katika mchezo wowote zaidi ya kutoka sare, leo imeushangaza umma na dunia kwa ujumla kwamba ni timu nzuri na inaweza kupamabana na timu yoyote.
Mashabiki wa soka walijitokeza kwa wingi leo kuipa sapoti timu ya Young Africans kutokana na kuwa na imani kwamba uwezo wa kikosi cha Young Africans umekamilika kila idara na ndivyo hali ilivyokuwa katika dakika 90 za mchezo.
Washambuliaji wa Young Africans walikosa nafasi zaidi ya nne kipindi cha kwanza kutokana na kutokua makini na kukuta mashuti yao yakiokolewa na walinzi wa Ah Ahly na mlinda mlango wao Sherif Ekramny.
Mpaka dakika 45 za kipindi cha kwanza zinamalizika, Young Africans 0 - 0 Al Ahly.
Kipindi cha pili kilianza kwa timu zote kufanya mabadiliko kwa lengo la kuhakikisha wanapata mabao ya mapema lakini mabadiliko hayo yaliisadia Young Africans zaidi kuweza kumiliki mchezo na kutawala eneo la ulinzi.
Baada ya Young Africans kufanya mashambulizi langoni mwa Al Ahly mlindao mlango Ekramny alianza kupoteza muda huku wachezaji wa ndani ndao wakijiangusha mara kwa mara wakifikira kupoteza muda na mchezo kumalizika kwa sare.
Dakika ya 82 ya mchezo kona iliyopigwa na Saimon Msuva ilitua kichwani kwa Nahodha Nadir Haroub "Cannavaro" na kuukwamisha wavuni na kuwaacha mabingwa watetezi Al Ahly na benchi la Ufundi wakiduwaa.
Bao hilo liliamsha shangwe kwa washabiki, wapenzi na wanachama kwa ujumla na kuwafanya Al Ahly kupoteana uwanjani na kama umakini wa washambuliaji wa Young Africans ungekua makini basi wangeweza kuongeza bao la pili.
Mpaka dakika 90 za mchezo zinamalizika, Young Africans 1 - 0 Al Ahly.
Mara baada ya mchezo kocha wa Young Africana amesema anashukuru vijana wake wamecheza vizuri mchezo wa leo, walipata nafasi nyingi lakini walishindwa kuzitumia na kutumia nafasi moja iliyopelekea kupata bao hilo la ushindi.
Kocha Hans amesema ameona mapungufu yaliyojitokeza katika mchezo wa leo watayafanyia kazi kuanzia jumatatu mchana kabla ya safari ya kuelekea Cairo nchini Misri katikati ya wiki tayari kwa mechi ya marudiano siku ya jumapili Januari 09 mwaka huu.
Young Africans: 1.Deo Munish "Dida", 2.Mbuyu Twite, 3.Oscar Joshua, 4.Nadir Haroub "Cannavaro", 5.Kelvin Yondani, 6.Frank Domayo "Chumvi", 7.Saimon Msuva, 8.Haruna Niyonzima, 9.Emmanuel Okwi, 10. Mrisho Ngasa/Said Bahanuzi, 11.Hamis Kiiza/Didier Kavumbagu 
 
Top