YAYA Toure yupo nchini Qatar kupata matibabu ya ugonjwa usiofahamika kabla ya kujiunga na Ivory Coast kwenye kambi ya maandalizi ya kombe la dunia nchini Marekani, shirikisho la Ivory Coast limesema jana ijumaa.
Yaya ni mchezaji pekee anayekosekana katika kikosi cha wachezaji 28 kilichotajwa na kocha Sabri Lamouchi kwa maandalizi ya awali ya kombe la dunia yaliyoanza alhamisi mjini Dallas.
Kiungo huyo atakwea pipa kuelekea Marekani alhamisi ijayo ili kujiunga na wenzake, shirikisho limeongeza katika taarifa yake.
Scare: Yaya Toure is being treated for an injury before he meets up with Ivory Coast for the World Cup
Madaktari wa Hospitali ya Aspetar Orthopaedic na Sports Medicine mjini Doha wamethibitsha kulazwa kwa mwanasoka huyo bora wa Afrika kwa kile kilichoelezwa kuwa ni “Majeruhi ndogo`
Toure alipata majeruhi ya mguu katikati ya aprili, lakini alirudi uwanjani baada ya wiki mbili kuisaidia Manchester City kubeba ubingwa wa ligi kuu soka nchini England.
Katika mchezo wa mwisho ambao Man City waliifumua West Ham, mei 11 mwaka huu, Yaya alitolewa kipindi cha pili kwa madai kuwa alipata majeruhi ya nyama za paja.
Main man: The Ivory Coast fans will be hoping Toure will be fit for their team's World Cup challenge
 Mtu muhimu: Mashabiki wa Ivory Coast  wana matumaini ya kuona Toure anakuwa fiti kabla ya fainali za kombe la dunia.
 
Top