KOCHA wa Manchester Cuty, Manuel Pellegrini amethibitisha kuwa mshambuliaji wake, Sergio Kun Agero ataikosa mechi ya kesho jumatano dhidi ya Aston Villa katika dimba la Etihad baada ya kushindwa kuimarika majeruhi yake.
Mshambulaiji huyo raia wa Argentina alifunga bao moja katika ushindi wa mabao 3-2 dhidi ya Everton kwenye uwanja wa Goodison Park jumapili iliyopita, lakini alitolewa nje dakika ya 28 baada ya kuumia.
Aguero hajawa na msimu mzuri mwaka huu kutokana na kukumbwa na majeruhi ya mara kwa mara na sasa atakosa mechi ya kesho,.
Pia yuko hatarini kukosa mchezo wa kufunga msimu dhidi ya West Ham jumapili ya wiki hii.
“Kwa kweli majeruhi ni kwa Sergio Aguero. Hajaimarika kwa asilimia 100, kwahiyo hayupo katika kikosi cha kesho”. Alisema Pellegrini.
“Labda (Aguero) atapata nafasi jumapili. Tutaona jinsi atakavyoimarika wiki hii na kuona uwezekano wa kucheza”.
Baada ya sare ya 3-3 waliyoambulia Liverpool jana dhidi ya Crystal Palace, Man City watarejea kileleni kama watashinda mechi ya kesho dhidi ya Aston Villa.
 
Top