10262075_746424102046552_8052636705202952436_nNa Baraka Mpenja, Dar es salaam
MASHABIKI zaidi ya 15 wamefariki dunia katika mchezo wa Ligi Kuu nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) baina ya wapinzani wa jadi, AS Vita Club na TP Mazembe mjini Kinshasa baada ya kutokea vurugu uwanjani.
TP Mazembe ni klabu ambayo watanzania wawili, Mbwana Samatta na Thomas Ulimwengu huchezea, lakini wamenusurika na vurugu hizo zinazolaaniwa na wanamichezo wote duniani.
Vurugu hizo zilianza baada ya filimbi ya mwisho ya mchezo huo, huku TP Mazembe ikiongoza kwa 1-0 na Polisi walijaribu kutuliza ghasia hizo kwa kulipua mabomu ya machozi, lakini mambo yalikuwa magumu.
Mashabikiwa AS Vita ndio walioanzisha vurugu hizo kutokana na kutoridishwa na matokeo.
10346207_746424025379893_5649185486802586015_nMsemaji wa serikali ya DRC, Lambert Mende amesema uchunguzi wa tukio hilo la kuhuzunisha umeanza mara moja na kuna watu wengini 10 walijeruhiwa vibaya.
“Polisi wanne walishambuliwa na mashabiki walipolipua mabomu ya machozi na baadaye kukatokea vurugu kubwa na kusababisha vifo hivyo”. Waziri wa Kinshasa amewaambia Reuters news agency.
Mbaya zaidi kuna taarifa kuwa uwanja ulijaza mashabiki kuzidi uwezo wake, huku viongozi wakijua wazi kuwa huo ulikuwa mchezo wa mwisho katika michuano ya ligi kuu ya DRC.
Klabu hizo mbili ndizo zenye mafanikio zaidi nchini Congo na kihistoria kila zinapokutana huwa kunatokea vurugu na presha kubwa mashabiki wa wake.
Vurugu hizo zinatokea wakati TP Mazembe na AS Vita zimepangwa kundi moja katika Ligi ya Mabingwa Afrika na zitachuana tena Mei 25, mwaka huu mjini Lubumbashi.
 
Top