Na Baraka Mpenja, Dar es salaam
MWENYEKITI wa kamati ya uchuguzi ya Simba sc, Damas Ndumbaro anatarajia kukutana na waandishi wa habari kesho na kuweka hadharani majina ya wagombea wa nafasi mbalimbali katika uchaguzi wa juni 29 mwaka huu.
Katibu mkuu wa kamati ya uchaguzi huo, Halid Kamguna amesema mkutano huo utafanyika katika ukumbi wa Gymkan jijini Dar es saalam majira ya saa 11:00 asubuhi.
Kamguna aliongeza kuwa jana kamati ya uchaguzi ilikutana kumalizia zoezi la kuhakiki fomu za wagombeo wote wa nafasi za uongozi, hivyo majina yote yataanikwa kesho.
Moja ya wagombea waliokuwa kivutio kikubwa katika nafasi za juu ni Evance Aveva na Michael Richard Wambura waliochukua fomu ya kuwania Urais wa klabu hiyo.
Wagombea hawa waliteka hisia za wanachama wa klabu ya Simba waliowasindikiza kwa mbwembwe nyingi wakati wa kuchukua na kurudisha fomu.
Aveva na Wambura wanatarajiwa kuchuana vikali kwa kuangalia jinsi walivyosindikizwa na watu wengi wanaoaminika kuwa wanachama wa Simba. 
Nafasi ya makamuwa rais,Jamhuri Kiwhelo `Julio` alikuwa kivutio kikubwa, lakini wengine kama Geofrey Nyange Kaburu, na Joseph Itang`are `Mzee Kinessi` walijitosa pia.
 
Top