Na Baraka Mbolembole
Ni kweli, Mzee Arsene Wenger hakuhitaji huduma ya Cecs Fabregas mara baada ya klabu ya FC Barcelona kutangaza kuwa watamuuza nahodha huyo wa zamani wa Arsenal. Awali, Manchester United ilitajwa kumuhitaji kiungo huyo wa mashambulizi wakati David Moyes akiwa kocha wa United, Arsenal, Manchester City zilitajwa kuwepo katika vita ya kuwania saini ya mchezaji huyo wa timu ya Taifa ya Hispania, lakini kufikia leo, Fabregas ameonekana akiwa na jezi namba nne ( 4) ya Chelsea iliyoachwa wazi na mlinzi, David Luiz alijiunga na mabingwa wa Ufaransa, PSG.
Wakati usajili wa mshambuliaji, Diego Costa ukitajwa kukamilika, kocha, Jose Mourinho amekuwa bize kuhakikisha anafanya usajili wa wachezaji bora kuziba nafasi za nyota wanao ondoka kama Samuel Eto’o, Frank Lampard, Luiz. Fabregas akiwa na miaka 28 kwa sasa ameshindwa kuendana na soka la Barcelona katika misimu mitatu iliyopita baada ya kuondoka, Arsenal kwa ada ya pauni millioni 40. Chelsea imemsaini, Fabregas kwa pauni millioni 30 na biashara hiyo inaweza kutoa matunda mazuri kwa Chelsea ambao wamempata mchezaji mzoefu na mwenye kiwango cha juu.

Fabregas atavaa jezi namba 4 katika klabu ya Chelsea.
Fabregas aliondoka Arsenal mwaka 2011 baada ya kuichezea timu hiyo tangu mwaka 2004. Chelsea imemsajili mchezaji huyu wa timu ya Taifa ya Hispania kwa ada ya uhamisho wa pauni million 30 kutoka Barcelona. Hilo limetokea siku chache baada ya kumuongezea mshahara kiungo na mchezaji bora wa klabu hiyo ya miaka miwili mfululizo, Eden Hazard. Fabragas anaweza kwenda sambamba na Hazard katika nafasi ya kiungo wa mashambulizi, Mourinho anajua sababu kubwa ya kukosa kikombe chochote msimu uliopita. Anaweza kuwalaumu sana washambuliaji wake, lakini mbinu zake za kulinda wakati mwingine huwa si nzuri hasa unapokutana na timu inayomiliki mpira na kutengeneza nafasi.
Fabregas ni kiungo mzuri katika kushambulia, kupiga pasi za magoli na mchezesha timu mwenye pasi za timilifu, alishindwa kutulia katika klabu ya Barcelona katika kipindi cha misimu mitatu iliyopita. Ila uwezo wake wa kumudu soka la Kiingereza na katika umri wa miaka 28 aliyonayo sasa, mchezaji huyo anaweza kushangaza kwa soka lake la kasi na pasi zenye macho . Nemanja Matic, nafikiri huu utakuwa wakati wake wa kucheza katika kikosi cha kwanza cha Chelsea, atafaa zaidi kucheza nyuma ya Fabregas na Hazard na watatu hao wanaweza kuibadili Chelsea kiuchezaji na kuficha pengo ambalo linaweza kuwasumbua kwa muda mrefu la kumkosa Lampard kama Mourinho ataendelea kuichezesha timu yake katika mfumo uleule wa siku zote, Kujilinda na kushambulia kwa kushtukiza.
- See more at: http://shaffihdauda.com/?p=1962#sthash.tnJ0eRbF.dpuf