Anawindwa: Kocha wa zamani wa Manchester United alionekana mwenye furaha baada ya kugusa ardhi ya Istanbul.
DAVID Moyes amepewa ofa ya mwaka mmoja wenye thamani ya paundi milioni 4 ili arithi mikoba ya Roberto Mancini katika nafasi ya kocha mkuu wa Galatasaray.
Moyes anarudi kazini mapema baada ya kufukuzwa Manchester United mwezi aprili mwaka huu baada ya kufanya kazi kwa miezi tisa tu katika mkataba wake wa miaka mitano.
Katika utawala wake Man united, Moyes alishindwa kuipa makali baada ya kurithi mikoba ya Sir Alex Ferguson aliyestaafu kufundisha soka.
Moyes alishawasili mji mkuu wa Uturuki na kufanya mazungumza na leo hii jumamosi nchini kwake Scotland.
Mazungumzo ya pande mbili yamekwenda vizuri na kuwaacha Waturuki wakiamini kuwa tayari wameshamnasa mtu wao.
Anawasili: David Moyes alikuwa mjini Istanbul, lakini inafahamika kuwa tayari dili la kujiunga na klabu ya huko limekamilika.
Hana shida: Tangu afukuzwe kazi Manchester United, David Moyes amekuwa akila maisha Miami
Jurgen Klinsmann (kushoto) na Joachim Low (kulia) wanawindwa zaidi na Galatasaray.
Galatasaray ndani, Fenerbahce nje
Licha ya kumaliza nafasi ya juu katika ligi kuu ya Uturuki msimu uliopita, Fenerbahce hawatacheza UEFA wala ligi ya Europa msimu ujao.
Mwezi Julai 2012, UEFA iliwafungia kutoshiriki michuano ya Ulaya kwa misimu miwili baada ya kukutwa na hatia ya kupanga matokeo.
Wakala wa Uturuki, Muzzi Ozcan aliyeshughulikia suala la Mancini alisafiri kutoka London kwenda Istanbul jana ijumaa kwa ajili ya kukamilisha dili hilo.
Mwezi Julai 2012, UEFA iliwafungia kutoshiriki michuano ya Ulaya kwa misimu miwili baada ya kukutwa na hatia ya kupanga matokeo.
Wakala wa Uturuki, Muzzi Ozcan aliyeshughulikia suala la Mancini alisafiri kutoka London kwenda Istanbul jana ijumaa kwa ajili ya kukamilisha dili hilo.
Galatasaray walithibitisha kuwepo kwa kikao baina ya rais wa klabu, Unal Aysal na Moyes, lakini mazungumzo yalikuwa ni kubadilishana mawazo na walisema Joachim Low na Jurgen Klinsmann ndio makocha wanaowahitaji.
“Rais ameshatoa hotuba juu ya hilo,” alisema msemaji wa Galatasaray.
“Alisema kwamba tumezungumza na David Moyes na alisema kwamba yeye sio chaguo la Galatasaray”;
“Walikuwa wanabadilishana mawazo tu. Ni kweli Rais amezungumza na David Moyes”.
‘Hatuna haraka, tunasubiri kombe la dunia limalizike. Watu wawili tunaowataka ni Low au Klinsmann.’.