Selecao walihangaika kuvunja ngome imara ya Serbia katika dimba la Sao Paulo mpaka Fred alipofanikiwa kupenya katika dakika ya 58 na kufunga bao hilo pekee.
Mashabiki walikosa uvumilivu na kujikuta wakiwazomea wachezaji wao kwa soka `mbofu mbofu` dhidi ya Serbia, lakini Scolari hana tatizo na kitendo hicho.
“Ni kitu cha kawaida,” Kocha huyo aliwaambia waandishi wa habari wa Brazil. “Ilitokea Goiania na sehemu nyingine”.
“Haikuwa tatizo kwa mchezaji wangu yeyote. Wako tayari kwa hili”.
“Lakini baada ya filimbi ya mwisho, asilimia 65 ya mashabiki 67,000 waliridhishwa”.