KOCHA wa Chelsea, Jose Mourinho amesema haogopi ujio wa Louis van Gaal baada ya kutambulishwa rasmi katika klabu ya Manchester United siku ya alhamisi ya wiki hii.
Wawili hao waliwahi kufanya kazi kwa miaka mitatu wakati wakiwa Barcelona na Mourinho anasema anaangalia mbele kukabiliana na mashetani wekundu kwenye mechi za ligi kuu.
“Simuogopi yeye kuwepo hapa,” aliwaambia Mail on Sunday.
“Naangalia mbele kucheza dhidi ya United. Hakuna kinachonitisha mimi. Nilimuangalia kwenye mkutano wake na waandishi wa habari, alikuwa Van Gaal wa kweli, mkweli na muwazi, mara zote yuko hivyo”.
Van Gaal alishinda makombe akiwa na Barcelona, Bayern Munich na Ajax katika maisha yake ya soka na Mourinho amesema kocha huyo atafanya kazi nzuri Old Trafford.
“Ni kocha mzuri, mzuri sana, atakuwa mkubwa kwa Manchester United. Wote ni makocha wakubwa”.
“Tulizaliwa ili tufanye hivi. Louis alikuwa kocha bora kombe la dunia na ni kocha rafiki wa maisha”.
“Ninamheshimu sana mtu huyu. Amekuwa na mafanikio makubwa katika kazi yake. Katika kazi ya Kufundisha, kama unakabiliana na kushinda au kupoteza, hiyo ni njia sahihi, utaimarika”