article-2681224-1F66B2F100000578-76_634x756

NYOTA wa Brazil, Neymar,  ataikosa mechi ya nusu fainali baina ya wenyeji dhidi ya Ujerumani jumanne ijayo, hii ni kwa mujibu wa kocha, Luiz Felipe Scolari.
Taifa mwenyeji limefanikiwa kufuzu hatua ya nusu fainali baada ya ushindi wa mabao 2-1 mjini Fortaleza, lakini nyota wake alitolewa nje kwa machela dakika tatu kabla ya mechi kumalizika na amekimbizwa hospitali baada ya mechi kumalizika kutokana na kupata majeruhi ya mgongo.
Neymar amekuwa akijikaza kuimarika katika mechi zote za Brazil kutokana na majeruhi ya  goti, lakini alifaulu kuanza katika mechi zote.
Agony: Neymar lies in agony after being kneed in the back just three mintues from the end
Neymar akiwa amelala chini baada ya kupata majeruhi ya mgongo dakika tatu kabla ya mechi kumalizika. 

none
Cynical: With the ball nowhere near Juan Zuniga smashes his knee into the lower part of Neymar's back

End of the line? Neymar is carried down the tunnel amid fear that his World Cup could be over
 Mshambuliaji huyo wa Barcelona amefunga mabao manne katika fainali za mwaka huu, lakini alishindwa kuongeza dhidi ya Colombia kabla ya kutolewa nje kwa machela dakika tatu kabla ya mechi kumalizika.
Kocha wa Brazil Luiz Felipe Soclari alisema: “Sidhani kama ataweza kucheza mechi ijayo”.
“Amekimbizwa hospitali binafsi na madaktari kwasababu aligongwa na goti katika mgongo wake”.
” Alikuwa analia kwa maumivu. Haitakuwa rahisi kwake kuimarika kwa kuzingatia ukweli kwamba ni majeruhi ya mgongo na maumivu aliyonayo ni makubwa. Acha tuwe na matumaini kuwa kila kitu kinakwenda vizuri
 
Top