TAARIFA
zilizotufikia hivi punde zinaeleza kuwa baraza la vyama vya michezo kwa ukanda
wa Afrika mashariki na kati, CECAFA limekikataa kikosi B cha klabu ya
Yanya kilichopelewa kushiriki michuano ya kombe la Kagame inayotarajia
kuanza kushika kasi Agosti 8 mwaka huu, mjini Kigali, nchini Morogoro.
Imeelezwa
kuwa Yanga wanatakiwa kubadilisha kikosi hicho kufikia alfajiri ya kesho na
kama haitafanya hivyo, basi timu itatolewa kwenye mashindo.
Aidha,
Taarifa hizo zinafafanua kuwa kama Yanga watashindwa kutekeleza maamuzi hayo,
basi mabingwa wa ligi kuu soka Tanzania bara, Azam fc watapewa nafasi hiyo.
Tangu
awali CECAFA walisema Azam itapewa nafasi ya upendeleo, lakini mpaka sasa wana
Lambalamba hawajapewa taarifa rasmi.
Kocha
wa Azam fc, Mcameroon, Joseph Marius Omog alisema kama atapata nafasi ya Kombe
la Kagame itakuwa nafasi nzuri ya kufanya maandalizi ya ligi kuu na ligi ya
mabingwa barani Afrika.