Tembo: Didier Drogba akipiga shuti kujaribu kufunga goli baada
ya kuingia katika dakika za lala salama
MBWATUKAJI Jose Mourinho ameanza ligi kuu England ‘Swafii’
kabisa baada ya kufanikiwa kuingoza ugenini Chelsea kupata ushindi wa mabao 3-1
dhidi ya timu mpya ya Burnley.
Wenyeji ndio walikuwa wa kwanza kuandika bao la kuongoza katika
dakika ya 15 kupitia kwa Scott Arfield, lakini mshambuliaji mpya wa
Chelsea, Diego Costa alifungua akaunti ya mabao katika mechi za ligi kuu baada
ya kuifungia timu yake bao la kusawazisha katika dakika ya 17.
Akaunti ya magoli: Diego Costa akifunga bao lake la kwanza la
ligi kuu
Wakati Burnley wakiwa na matumaini ya kuongeza bao,
Mjerumani, Andre Schurrle aliifungia Chelsea bao la kuongoza katika dakika
21 na Branislav Ivanovic akahitimisha karamu ya mabao katika dakika ya 34.
Tatizo kubwa kwa Burnley ni kwamba wachezaji wake hawajawahi
kukutana na kitu kama hiki, hivyo kujikuta wakizidiwa maarifa kimbinu na
kiufundi.
Hadi beki yumo: Ivanovic akifunga goli la tatu
Mabingiwa hao wa The Championship, mara kwa mara waliambiwa
ligi ni ngumu lakini sio ngumu kama hivi leo.
Katika mechi ya leo, Didier Drogba alianzia benchi na kucheza
mechi ya kwanza tangu arudi Chelsea, lakini alishawahi kucheza mechi ya kwanza
kabisa miaka ya nyuma.
Mlinda mlango, Thibaut Courtois naye alimkalisha kwenye ‘gogo;
mkongwe Petr Cech.
Mambo kutoka kwa Mjerumani: Andre Schurrle akiifungia
Chelsea bao la pili
Kikosi cha Burnley: Heaton, Trippier, Duff, Shackell, Mee,
Taylor (Kightly 70), Marney, Jones, Arfield, Ings (Sordell 82), Jutkiewicz
(Barnes 70).
Wachezaji
wa akiba: Wallace, Gilks, Long, Dummigan.
Kadi
ya njano: Sordell.
Kikosi cha Chelsea: Courtois, Ivanovic, Cahill,
Terry, Azpilicueta, Fabregas, Matic, Schurrle (Willian 78), Oscar (Mikel 82),
Hazard (Drogba 84), Costa.
Wachezaji
wa akiba: Cech, Luis, Zouma, Torres.
Kadi
ya njano: Costa.