Ni kama sinema hivi lakini ukweli usajili wa mshambulizi wa kimataifa wa Uganda, Emmanuel Okwi katika kipindi cha miaka miwili kimeonyesha udhaifu mkubwa wa viongozi wa klabu kubwa nchini Tanzania. Wakati, Simba SC na Yanga SC wakishindwa kukamilisha usajili wao katika ‘ muda mwafaka’, kuna mashindano ambayo kambi ya Simba walikuwa wakijaribu kuyafanya ili kuonyesha baadhi ya nguvu zao zilizowafanya kuwa viongozi wa klabu kubwa hiyo. Yanga ‘ walishamaliza mchezo’ mwezi mmoja uliopita. Mwalimu, Marcio Maximo tayari anajua ni wachezaji gani wa kigeni ambao anaweza kufanya nao kazi kwa manuu ya Yanga. Okwi hakuwa katika mipango ya Maximo ndiyo maana ‘ kiurahisi’ tu Yanga wameamua kuachana naye miezi sita baada ya usajili wa ‘ mbwembwe’ mwezi Disemba, ambao uliambatana na bao ‘ kali’ dhidi ya timu yake ya zamani ( wakati huo katika mchezo wa Matani Jembe’. Rais wa klabu ya Yanga, Yusuph Manji amesema hawana kinyongo kwa mchezaji huyo kujiunga na mahasimu wao, lakini ni lazima taratibu zifuatwe. Kuna gharama nyingi ambazo Simba watalazimika kuzilipa ikiwa wanamuhitaji Okwi kwa mara ya pili. UKiachana na mapenzi ya kiushabiki na kurudi katika uhalisia wa mambo, katika hili ni lazima taratibu zifuatwe. Yanga ni timu pekee ambayo ilikuwa na uwezo wa kumsaidia Okwi kutoka katika ‘ kitanzi kizito’ cha Etoile du SAlehe ya Tunisia klabu ambayo ilikuwa katika mgogoro mkubwa wa kisheria na mchezaji huyo wa timu ya taifa ya Uganda. Wakati akitambulishwa kwa mara ya pili mbele ya waandishi wa habari siku ya jana mchezaji huyo alisema kuwa aliuomba uongozi wa Simba kumsaini wakati huu akiwa katika kesi dhidi ya Yanga ambao wamefungua katika Shirikisho la soka, Simba wala hawajafikiria mata mbili. Cha ajabu alitambulishwa mchezaji wa ‘ muda usiojulikana’. Kwa hiyo mkataba huo unaweza kuwa hata wa siku mbili! Haya ndiyo maajabu ya soka la Tanzania. Kulikuwa na ulazima wa Simba kumtema Donald Musoti kwa sababu tu ya Okwi? Yanga hawakuwa na haja naye kwa sababu mchezaji huyo alichangia kwa kiasi kikubwa timu hiyo kukosa ubingwa wa ligi kuu licha ya kupewa zaidi ya million 100 wakati akisajiliwa kwa lengo la kuisadia timu hiyo katika michuano ya kimataifa. Ni mchezaji mwenye kipaji kikubwa ndiyo maana mashabiki na wapenzi wa timu hiyo walijitokeza kwa wingi kumpokea wakati alipotua nchini mwishoni mwa mwaka uliopita.Okwi alikosa michezo sita ya ligi kuu na Yanga walipambana kuhakikisha anakuwa huru na hilo lilitokea licha ya mchezaji huyo kukosa michezo mitatu ya mwanzo katika klabu bingwa Afrika, mapema mwaka huu. Je, Yanga wanafurahia tena kipaji ‘ walichokiamini ni chao’?. Wapi, hakuna kitu kama hicho, mashabiki wa Yanga hawana furaha kwa sasa kwa sababu ‘ wamesalitiwa’ na mtu waliyemuamini. Okwi hana ‘ busara’ licha ya hilo ni kijana mdogo ambaye anachenguliwa na ‘ usajili wa fasheni’ unaotawala nchini. Angecheza wapi katika kikosi cha Yanga?. Hana nafasi yoyote kwa sababu hakujitoa moja kwa moja kwa timu hiyo. ‘ Yanga wamemnunua wapi, Emmanuel Okwi’. Sikuwahi kuamini tangu wakati ule, kwa sababu Okwi hakuletwa Yanga kwa sababu za kimpira. Yule aliyepigani kusajiliwa kwake hayupo tena klabuni, Yanga wamefanya ‘ maamuzi babu-kubwa’ na wataendelea kufurahia maendeleo ya timu yao kuelekea msimu mpya. Simba bado wanapepesuka, wanafanya mambo ambayo yatawaondoa mapema nje yam bio za ubingwa msimu ujao kwa ‘ kulipua, lipua mambo’. Yuko wapi, Hussein Butoyi?. Okwi ataisadia sana Simba ndani ya uwanja endapo mambo yake yatakwenda vizuri na kuruhusiwa kuichezea timu hiyo ambayo aliifungia mabao 12 msimu wa 2011/12 walipotwaa ubingwa wa mwisho wa ligi kuu. Simba wamemsani kwa mkataba wa muda usiojulikana, lakini wanaamini tifauti kuhusu OKwi. Bado wana fikra zilezile kuwa OKwi ni mchezaji bora zaidi ya ‘ Yule aliyefunga bao kali’ dhidi ya Entente Setif katika dakika ya mwisho kabisa ya mchezo na kuvusha timu yake hadi hatua ya 16 bora ya kombe la Shirikisho barani Afrika, April, 2012. Okwi ni kijana anayeendelea kukua na Yanga wanasema walikuwa na mkataba naye hadi mwaka 2016 Hivyo Simba watalazimika kulipa fidia ya mshahara wa mika yote hiyo ambayo Okwi alitakiwa kuitumikia Yanga, gharama ambayo inafikia millini 288. Okwi amecheza mpira wa ushindani kwa miaka mitano tu tangu aliposajiliwa kwa mara ya kwanza na SC Villa akiwa kinda wa miaka 17 na kufunga mabao 16 katika ligi kuu ya Uganda mwaka 2009. Alinunuliwa na Simba na akaitumikia kwa muda wa miaka mitatu na nusu akitwaa mataji mawili ya ligi kuu Tanzania Bara, msimu wa 2009/10 na 2011/12. Simba ilikuwa ipate zaidi ya million 300 kama mchezaji huyo angetulia Tunisia baada ya kuuzwa kwa Etoile, Yanga wametumia zaidi ya millioni 100 kumfanya Okwi kuwa huru, Simba watalazimika kuwalipa Yanga zaidi ya million 280 ili kupata huduma ya Okwi. ‘ Pwagu na Pwanguzi’, ‘ Kulwa na Dotto’ Okwi si biashara nzuri kwenu. Safi Yanga kuachana naye, Geilson Santos alikuwa muhimu zaidi ya Mganda huyo katika mipango ya Maximo, Simba wanafikiri Okwi ni yuleyule tu, alikuwa akimburuza mmoja wa makocha wasaidizi wa Yanga, Shadrack Nsajigwa. Yanga watapata faida katika biashara ya OKwi, Simba wajikamuae na mkataba wao wa muda usiojulikana - See more at: http://shaffihdauda.com/?p=5611#sthash.f8yec0BD.dpuf
EMMANUEL OKWI ANAVYOHAMA KIRAHISI SIMBA SC, YANGA SC