Diego Costa amefunga mabao mawili katika michezo miwili ya mwanzo akiwa na klabu ya Chelsea katika ligi kuu ya England ambayo itaingia kati tika wiki ya tatu wikendi ijayo. Kikosi cha kocha, Jose Mourinho kilipambana na kusawazisha bao la dakika ya 14 katika mchezo dhidi ya Burnley kisha kuchomoza na ushindi wa mabao 3-1 katika uwanja wa ugenini. Washambuliaji, Costa, Andre Schurrle walifunga katika mchezo, huku Eden Hazard akifanya hivyo katika mchezo dhidi ya Leicester City wiki iliyopita ‘ The Blues’ waliposhinda kwa mabao 2-0 katika uwanja wa Stamford Bridge.
GOODSON PARK…
Everton inacheza soka la kasi, nguvu, na wachezaji wa safu ya mashambulizi ni ‘ wauaji wasiotabirika’. Kikosi cha kocha, Robert Martinez kimeshindwa mara mbili kulinda uongozi katika michezo miwili ya mwanzo. Mara mbili ‘ Toffee’ walipoteza uongozi katika mchezo wa ugenini dhidi ya Leicester siku ya ufunguzi na kujikuta wakipata sare ya kufungana mabao 2-2. Mshambulizi ghali zaidi katika klabu hiyo, Romelu Lukaku hajafunga bao lolote lakini timu hiyo imekuwa ibebwa na mshambulizi, Steven Naismith ambaye amefunga mabao mawili katika michezo miwili iliyopita likiwemo lile dhidi ya Arsenal katika uwanja wa Goodson Park, wiki iliyopita walipolazishwa sare ya kufungana mabao 2-2 na Arsenal.
Everton ilikuwa mbele kwa mabao 2-0 hadi mchezo ulipokuwa umesalia dakika saba umalizike. Arsenal ‘ wakatumia ukubwa wao’ kusawazisha mabao hayo na kutengeneza sare ya ‘ maajabu’. Dhidi ya Chelsea, Jumamosi hii itakuwa mechi ngumu kwa kila upande. Kikosi cha Jose kipo katika mwendo wa asilimia ya ushindi, wakati Martinez akitafakari namna ya kuziba ‘ nyufa’ katika safu yake ya ulinzi ambayo imeruhusu mabao manne katika michezo miwili iliyopita.
Chelsea imepoteza michezo miwili katika safari tatu za mwisho ‘ Merseyside’, ushindi wao wa mwisho walipata, 30 Disemba, 2012 baada ya kushinda kwa mabao 2-1 yaliyofungwa na Frank Lampard katika dakika za 42 na 72 akifuta bao la mapema dakika ya pili lililofungwa na kiungo, Steven Piener. Jose alishuhudia timu yake ipoteza mchezo wa kwanza msimu uliopita baada ya kukubali kipigo cha bao 1-0, 14 Septemba kwa bao la dakika ya 45 lililowekwa kimiani na Naismith.
Safari hii Jose anakwenda akiwa katika umbo zuri na atakutana na washambuliaji ‘ aliowakaa kiana’ , Lukaku na Samuel Eto’o ambaye amekamilisha usajili wa kujiunga na Everton, Jumanne hii. Jose aliamua kumuacha Eto’o licha ya mchezaji huyo kufunga mabao tisa katika uwanja wa Stamford Bridge msimu uliopita. Lukaku ameuzwa kwa Everton baada ya nafasi yake kukosekana katika safu ya mashambulizi ya Chelsea ambayo ina washambuliaji wa uhakika.
Didier Drogba ana umri wa miaka 36 lakini amesajiliwa ili kuongeza uzoefu katika safu ya mbele. Jose alimuacha huru Eto’o huku akimpiga kijembe, Mcameroon huyo kwa kumuita ‘ Mzee’. Lakini amemsaini, Drogba mwenye miaka mitatu zaidi ya Eto’o.
Didier Drogba ana umri wa miaka 36 lakini amesajiliwa ili kuongeza uzoefu katika safu ya mbele. Jose alimuacha huru Eto’o huku akimpiga kijembe, Mcameroon huyo kwa kumuita ‘ Mzee’. Lakini amemsaini, Drogba mwenye miaka mitatu zaidi ya Eto’o.
Kipigo kwa mara nyingine, Goodson Park kinawezekana kutokea kwa Chelsea ila si kazi rahisi kwa Martinez kumshinda, Jose kwa mara nyingine ukizingatia tayari amefanya marekebisho makubwa katika kikosi. Drogba na Costa wamechukua nafasi za Eto’o na Demba Ba, Cecs Fabregas ametua na mchezaji huyo wa nafasi ya kiungo ameonyesha kiwango cha juu katika michezo miwili iliyopita. Cecs ni mbadala sahihi wa Lamps, Luiz Filipe amesajiliwa kuongeza nguvu katika ngome. Jose ni kocha mwenye mbinu nyingi za kusaka ushindi iwe anacheza katika uwanja wa nyumbani au ugenini ila ni mbinu gani atazitumia dhidi ya Everton wikendi hilo lipo katika akili yake mwenyewe lakini kichwa kitamuuma kuwazuia wachezaji wake wa zamani wasimtie katika aibu ya kuwa mteja mbele ya Martinez.