JOSE Mourinho amekuwa akikosolewa kwa kumuacha mshambuliaji kijana kuondoka Chelsea, lakini Pete Hall anasema The Blues wamepata doa.
Baada ya kushika nafasi ya tatu katika orodha ya wafungaji wa ligi kuu msimu uliopita (nyuma ya Robin van Perise na Luis Suarez), watu wengi wamekuwa na maswali kuwa ni kitu gani Lukaku angefanya ili kupata nafasi ya kucheza Chelsea.
Kufunga zaidi ya mabao 10 kwa msimu ni kitu ambacho Diego Costa aliyesajiliwa amefanya mara moja, wakati Lukaku amefunga mabao kama hayo mara nne licha ya kutoaminiwa katika maisha yake ya soka.
Akiwa ameichezea Chelsea ligi kuu kwa dakika 199 tu tangu ajiunge miaka mitatu iliyopita kutokea Anderlecht, ilikuwa rahisi kwa klabu hiyo ya London Magharibi kumuuza baada ya dau la paundi milioni 28 kuwekwa mezani.
PESA NDIO MUHIMU
Kama sehemu ya kuweka sawa mahesabu wakati huu wa sheria ya matumizi ya fedha kwa Chelsea. Jose Mourinho hajaona tatizo kumuuza nyota kijana anayechipukia. Anajua wazi kuwa kuendelea kumlipa hela mchezaji asiyemtumia ni hasara kuliko kumuuza moja kwa moja.
“Ni kijana mdogo anayependa kuzungumza. Lakini kitu pekee ambacho hakusema ni kwanini alienda kwa mkopo Everton,” Mourinho alisema mwezi desemba alipokuwa anazungumzia hatima ya Mbelgiji huyo.
Imeaminika kuwa Mreno huyo hana nia ya dhati kwa vijana baada ya kumuuza Lukaku na kumuacha Fernando Torres licha ya kufunga kwa asilimia 13.51 kwa nafasi alizopata misimu miwili iliyopita.
Mabao 71 ya Chelsea msimu uliopita yalikuwa machache zaidi ukilinganisha na ya mabingwa watetezi Manchester City, lakini Costa ameletwa kumaliza tatizo hilo akiwa amafunga mabao 27 na Atletico Madrid msimu uliopita na kuisaidia kutwaa ubingwa wa La Liga.
HAKI YA KUUZA
Wakati mjadala unaendelea kama Mourinho atajuta kumuuza nyota huyo, klabu imenufaika na dau walilopata katika mauzo ya Lukaku.
Paundi milioni 50 walizotumia misimi miwili iliyopita zimejaribu kupunguzwa. Shukurani kwa Mourinho kwa kumsajili Diego Costa, Filipe Luis na Cesc Fabregas.
Ukilinganisha na wapinzani wao Manchester United ambao walilundika paundi milioni 112 kwa miaka miwili iliyopita, ilikuwa faida sana kwa kulinganisha na matumizi makubwa ya Chelsea katika soko la usajili.
Asernal licha ya kulaumiwa na mashabiki wake kutosajili, ilitumia paundi milioni 92 ndani ya miaka miwili iliyopita.
Wakati huo huo, vikwazo alivyowekewa mmiliki wa Manchester City Sheikh Mansour baada ya kutumia fedha nyingi katika usajili kinyume na sheria ya matumizi ya fedha, inaonekana kuwaogopesha wengi.
Mourinho aliogopa zaidi kwasababu baada ya kumsajili Drogba, alibakiwa na nafasi moja ya mchezaji wa kigeni.