Baraka Mbolembole, Dar es Salaam,
Rais wa klabu ya Yanga, Yusuph Manji amesema kuwa klabu yake itawasilisha orodha ya wachezaji sita wa kigeni badala ya watano wanaotakiwa kwa mujibu wa kanuni za usajili.
Akizungumza na vyombo vya habari siku ya leo, Manji amesema kuwa majina hayo yataambatana na jina la mshambulizi, Emmanuel Okwi ambaye jana klabu ya Simba SC ilitangaza kumsaini kwa mkataba wa muda usijulikana.
Mbuyu Twite na Haruna Niyonzima kutoka nchini Rwanda, Andrey Coutinho na Geilson Santos ‘ Jaja’ kutoka nchini Brazil na Hamis Kizza ni majina mengine matano ambayo yatapelekwa kwa shirikisho la soka nchini TFF, siku ya kesho.
HAYA NDIYO MALALAMIKO RASMI YA YANGA KUHUSU USAJILI WA OKWI