10copy
KIKOSI cha pili cha Azam fc kimepigwa mabao 2-0 dhidi ya Mtibwa Sugar katika mechi maalumu ya kirafiki ya Tamasha la Usiku wa Matumaini usiku huu uwanja wa Taifa, uliopo maeneo ya Chang’ombe, jijini Dar es salaam.
Kwa ushindi huo, wakata miwa wa mashamba ya Manungu Turiani Mkoani Morogoro wamefanikiwa kutwaa Ngao ya Matumaini.
Katika mchezo huo ambao ulikuwa maalumu kwa kocha mkuu wa Mtibwa, Mecky Mexime kuonesha wachezaji wake jinsi walivyoiva, wachezaji wawili wakongwe, Musa Hassan Mgosi na Vicent Barnabas walionesha kandanda la kuvutia na kudhihirisha kuwa utu uzima dawa.
Baada ya mechi ya leo , kikosi hicho cha Azam kitasafiri muda wowote kuelekea mjini Kigali  nchini Rwanda kikifuata kikosi cha kwanza kinachoshiriki kombe la Kagame
 
Top