Kaburu alisema baada ya kukamilisha usajili wa wahezaji hao kwa sasa nguvu wanaziamishia kwa wachezaji Poul Kiongera wa KCB ya Kenya na Jean Claude Hiranzi
SIMBA imeendelea kukiimarisha kikosi chake kwa ajili ya kujiandaa na Ligi Kuu msimu ujao huku uongozi wa timu hiyo ukikimbizana na muda wa usajili uliobakiza wiki mbili kabla ya kukamilika.
Zoezi la usajili kwa timu zinazo shiriki Ligi Kuu,linakamilika Agosti 17,na klabu ya Simba kupitia kwa Makamu wake wa Rais Geofrey Nyange Kaburu,amesema bado wanaendelea kufanya usajili kwa ajili ya kutaka kukiimarisha kikosi chao kabla ya zoezi hilo kufika mwisho.
Goal ilimeshuhudia Makamu wa Rais wa timu hiyo Geofrey Nyange Kaburu,akiwatambulisha wachezaji wawili Elias Maguli na Shabani Kisiga huku pia ikimpokea mchezaji Pierre Kwizere,raia wa Burundi kutoka timu ya Afu Abidjan ya Avory Coasty kwa ajili ya kusaini naye mkataba wa miaka miwili.
“Bado tunaendelea na zoezi hili la usajili kuhakikisha tunakiboresha kikosi chetu kwa kusajili wachezaji ambao tunadhani watakuwa na msaada kwetu kwa kushirikiana na kocha mkuu Zdravko Logarusic,”alisema Kaburu.
Kaburu alisema baada ya kukamilisha usajili wa wahezaji hao kwa sasa nguvu wanaziamishia kwa wachezaji Poul Kiongera wa KCB ya Kenya na Jean Claude Hiranzi ambapo mmoja wao wanaweza kumsajili ili aitumikie timu yao msimu unaokuja.
Hadi sasa Simba tayari imeshakamilisha usajili wa wachezaji sita wapya ambao ni kipa Husseni Sharifu na Shabani Kisiga’Malon’kutoka Mtibwa Sugar, Michael Mgimwa Mtanzania aliyekuwa anacheza soka la kulipwa kwenye klabu ya Roiet FC inayoshiriki ligi araja la pili nchini Thailand,Mohamed Husseni Tshabalala,kutoka Kagera Sugar,Elias Maguli kutoka Ruvu Shooting na Pierre Kwizera raia wa Burundi aliyekuwa akicheza soka kwenye klabu ya Afu Abidjan ya Ivory Coast.