Cristiano Ronaldo aliwaambia waandishi wa habari kuwa maisha yake ya baadaye yako Real Madrid baada ya kufunga magoli manne
CRISTIANO Ronaldo amejiweka mbali na taarifa zilizoenea kwamba anataka kurudi Manchester United.
Shujaa huyo wa magoli manne ya Real Madrid kati ya matano waliyoshinda jana usiku dhidi ya Elche, alikuwa na furaha kujibu maswali aliyoulizwa kuhusu United na Jose Mourinho.
Ronaldo alijibu maneno ya kocha wa Chelsea, Jose Mourinho aliyedai kuwa uhusiano wao umekwisha.
“Hii ni ishu isiyokuwa na umuhimu, ninachojali ni Madrid.” alijibu Ronaldo. “Ni mahala shwari kwangu mimi, nahitaji kuisaidia jezi hii. Kuhusu mambo haya sio wajibu wangu kuzungumza”
Alipoulizwa kuhusu tetesi za kurudi Man United, alisema: “Kuna tetesi nyingi kuhusu hatima yangu ya baadaye…hatima yangu ni Madrid. Nina furaha msimu huu kwasababu unakwenda vizuri, kuhusu hatima yangu sitasema, haina maana”