Welbeck taunts Man Utd: Arsenal a club on the up
Muonekano wa matumaini: Danny Welbeck amesisitiza kuwa yuko tayari kuonesha kipaji chake chote akiwa na Arsenal.
DANNY Welbeck amekiri kuwa alikuwa na ndoto za kuichezea Arsenal hata kabla ya kukamilisha usajili wake kwa dau la paundi milioni 16 siku ya mwisho ya dirisha la usajili, majira ya kiangazi akitokea Manchester United.
Welbeck amefichua siri hiyo katika mahojiano na tovuti ya Arsenal kuwa siku zote alikuwa anatamani staili ya uchezaji ya klabu hiyo na aliamini itafika siku ataingia Emirates.
Mshambuliaji huyo wa England pia alieleza furaha yake ya kukamilisha usajili wake.
Danny boy: Welbeck poses with his new No 23 shirt at Arsenal after his deadline-day move
“Ni muda wa furaha kwangu,’ alisema Welbeck. “Ni jambo kubwa kuwa sehemu ya klabu hii na ni timu ambayo niliitazama katika mechi za ligi kuu.Niliota kuichezea timu hii kabla. Hatimaye imetokea.


 
Top